ROMA MKATOLIKI, ALIKIBA WAIBUKA NA TUZO, DIAMOND PLATINUM ANG'ARA NA KUIBUKA NA TUZO TATU
Kulia ni Msanii Profesa Jay na kushoto ni Mkubwa Fella meneja wa kundi la TMK Family wakimkabidhi tuzo Roma Msanii wa muziki wa Hiphop aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hiphop.
Mwanamuziki Diamond akipiga picha na mama yake wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kutoka kulia pamona na wanenguaji wake mara baada ya kupokea tuzo yake ya utuzni bora wa nyimbo.
Mwimbaji wa muziki wa Taarab ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora kwa wanawake Malkia Khadija Omar Kopa akitumbuiza katika hafla hiyo usiku huu.
Malkia Khadija Omar Kopa akishukuru wapenzi wake mara baada ya kushinda tuzo ya mburudishaji bora, wa pili kutoka kushoto ni mume wake na wengine ni watoto wake.
Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora Kilimanjaro Music Award 2012 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania na nje ya nchi.
Msanii Nassib Abdul ‘Diamond’ usiku wa kuamkia leo ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award, baada ya kujinyakulia tuzo tatu.
“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo ninachukua tuzo ya tatu sasa hivi, alisema Diamond baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka, kupitia wimbo Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu usiku huu.
Diamond alizishinda nyimbo za Hakunaga ya Suma Lee, Wangu ya Jay Dee, Ndoa Ndoana ya Kassim na Bongo Fleva ya Dully Sykes
Mwanamuziki Diamond katikati akiwa jukwaani na wenzake kabla ya kuimba wimbo wa msondo katika hafla ya kukabidhi tuzo za wanamuzikii bora za Kilimanjaro Music Award zainazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kulia ni Khalid Chokoraa wa bendi ya mapacha watatu.
Kundi la THT likitumbuiza katika tuzo hozo usiku huu.
Mdau Kelvin Twisa ndani ya nyumba pia.
Meneja wa kinywaji cha Redds Vicktoria Kimaro akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Reviewed by crispaseve
on
07:46
Rating:












Post a Comment