Header AD

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAKABIDHI GARI MPYA AINA YA FORD FIGO KWA MSHINDI WAKE ISACK JUVENARY

Meneja wa bia ya Serengeti Lager Bw. Allan Chonjo kulia akikabidhi funguo za gari aina ya Ford Figo kwa mshindi wa gari hiyo katika Promosheni ya "Vumbua Dhahabu chini ya Kizibo" Bw. Isack Juvenary aliyojishindia hivi karibuni kutoka mkoani Morogoro, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika kwenye Duka la magari la CMC Motors lililopo katika barabara ya Azikiwe jijini Dar es salaam, katika picha wanaoshuhudia tukio hilo ni maafisa kutoka kampuni ya bia ya Serengeti
Meneja wa bia ya Serengeti Lager Bw. Allan Chonjoakizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi gari hilo, kulia ni mshindi wa gari hilo Isack Juvenary
Isack Juvenary akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti, wa tatu kutoka kushoto ni Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo
Bw. Isack Juvenary akifurahia gari yake huku akiwa haamini kilichotokea.
Bw. Isack Juvenary akifurahia gari yake huku akiwa amepozi pembeni mwa gari yake.
Isack Juvenary mwenye umri wa miaka 25 mkazi Morogoro ambaye ndiyo mshindi wa gari mpya aina FORD FIGO,Leo asubuhi katika ofisi za CMC zilizopo barabara ya azikiwe mkabala na jengo la maktaba square jijini Dar Es Salaam, amekabidhi wa zawadi yake hiyo ya gari na kushuhudiwa na vyomvo mbalimbali vya habari.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni ijulikanayo kama vumbua hazina chini ya kizibo. Promosheni hiyo inaendeshwa nchi nzima kwa wateja mbalimbali wa kampuni hiyo kujishindia zawadi za kila aina zikiwezo Magari. Bajaj, Pikipiki, Jenereta na zawadi zingine kemkem
Akiongea na wandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo amesema “Najisikia faraja kubwa sana ninapoona yale tuliyoyapanga kuyatimiza kwa wateja wetu kama SBL na kwamba hii ni sehemu tu ya yale yote tuliyopanga kufanya kwa jamii inayotuzunguka kwa kuthamini mchango wa wateja wetu na pia sisi tumelenga katika kuwapa mabadiliko katika maisha yao kwa kuzingatia mahitaji muhimu ya binadamu siku had siku. 
Ndiyo maana tuna zawadi za magari, Bajaji, majenerata na pikipiki ili ziwasaidie katika shughuli zao za kila siku na pia fedha taslimu kuanzia shilingi elfu kumi, elfu hamsini na laki moja ambazo unaweza kushinda alisema Chonjo huku akisisitiza kuwa promosheni hiyo bado inaendelea kwa wiki takriban saba zijazo na kuwataka watanzania wote wenye sifa zilizoainishwa katika vigezo na masharti vya promosheni hiyo kushiriki kwa wingi ili kuongeza uwezo wakushinda zawadi mojawapo.
Reviewed by crispaseve on 04:37 Rating: 5

No comments

Post AD