Mwananchuo wa chuo cha ualimu cha ST Aggrey kilichopo uyole jijini mbeya anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma zakuiba pikipiki zakusafirishia abiria maarufu kama bodaboda.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri kati 25 mpaka 30 .
Mgonja amesema tukio hilo limetokea mnamo july 2 mwaka huu majira ya saa 8 za mchana katika daraja lilopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara yakuelekea isanga jijini mbeya.
Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada yakupewa taarifa za kuibiwa kwa pikipiki yenye No T 438BZU aina T-BETTER yenye alama ya chama cha Demokrasia na maendeleo mali ya JOSEPH KAPASI(23)mkazi wa Ilomba jijini hapa
Kwaupande wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae alipoanza kuendesha vizuri alitokomea nayo na marabaada ya hapo alipatikana eneo la isanga akielekea barabara ya chunya ili aibe na ndipo akakamatwa na wanainchi wenye hasira kali nakuanza kumpa kichapo ambacho kimemfanya azirai. |
Post a Comment