Header AD

TIGO WAFANYA TAMASHA KUBWA JIJINI WASANII KIBAO WATOA BURUDANI

Profesa J, Wamitulinga Mchawi wa Rymes, nae hakujivunga ilimradi ni burudani na shwangwe mwanzo mwisho shoo ilianza saa 6:00 mchana hadi 12:00 jioni yani furahaaaaaaa teeeele.
Hapa maji yakazidi unga walianza kusukuma watu wanyuuuma abisa hapa wimbi la msukumano ndio linaishia yani ilikuwa kama maji baharini yanavyofanya mawimbi na watu walikuwa vivyo hivyo.
Joti hapa alipo lazimika kuchenji Staili yakupanda jukwaani mara hii hakufanya mbwembwe ndio akafanikiwa kudumu kwenye jukwaa hilo kwa dakika kumi tu, kabla mkanyagano haujaanza kwani kila alipoweka mbwembwe watu walianza kusukumana, mara kadhaa alijaribu kupanda jukwaani kwa mbwembwe msukumano unatokea hadi kusababisha jukwaa moja lililokuwa limewekwa  TV kubwa kwaajili ya kuonyesha fainali ya ulaya kuanguka na tv kuvunjika.
Sasa baada ya watu kutulia hapa anafanya vitu vyake.

Lakini punde tu mkanyagano ukaanza tena.

Huyu Mpoki naye akaja na Mpya akasema hivi "Sherehe fujo ndo yake kama walikuwa hawataki fujo sherehe yao si wangelifanya msikitini" Shangewe na nderemo zikalipuka na kuasababisha watu wote wafurahi kwani walishakasikirika kutokana na kuambiwa kuwa shoo ingevunjwa kutokana na vurugu.
Hapa Kijana wa TMK Juma Kassim Kiroboto AKA Juma Nature, akikamua vilivyo kwenye tamasha hilo na kusababisha mashabiki kumng'ang'ania asishuke aendelee kutumbuiza.

Farid Kubanda Fid Q, nae alikuwa semu ya burudani hiyo.

Profesa J, Wamitulinga Mchawi wa Rymes, nae hakujivunga ilimradi ni burudani na shwangwe mwanzo mwisho shoo ilianza saa 6:00 mchana hadi 12:00 jioni yani furahaaaaaaa teeeele.
Mzee wa kuongea na Mshua Eazy Busyness nae alipakua vitu vyake kwa mashabiki wake na hakuwaangusha kabisa aliwakilisha vilivyo tu.

Mzee wa kamua baba kamua baaaaaa, kamua baba usitumie iliziiiiii!

Mkanyagano ukaanza tena upyaaaaa.
Lakini pia walikuwepo waliopanda juu ya minazi ili washuhudie.

Roma Mkatoliki nae alikuwepo kwenye kimuhemuhe hiko na aliwakilisha vilivyo hakuwaangusha mashabiki wake.
Reviewed by crispaseve on 01:16 Rating: 5

No comments

Post AD