Header AD

WAZIRI MKUU ATAKA ALAT IKUNJUE MAKUCHA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ambako alifunga sherehe za maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa kitaifa kwenye uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza Julai 1, 2012. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Mhandishi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

Ataka iache kukaa kimya, ikemee uozo kwenye Serikali za Mitaa
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) iache kukaa kimya na badala  yake ikemee uozo unaofanywa na watendaji kwenye Serikali za Mitaa nchini.
 
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Julai mosi, 2012) wakati akifunga maadhimisho ya nane ya Siku ya Serikali za Mitaa yaliyofanyika  kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 
Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa Katiba ya ALAT, Jumuiya hiyo inao wajibu wa kuzisimamia Halmashauri kwa iliundwa ili kudumisha na kukuza maendeleo ya shughuli za Serikali za Mitaa Tanzania kwa kuondoa vikwazo na matatizo yote.
 
“Serikali za Mitaa zinakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa nilizozianisha ni ukusanyaji mdogo wa mapato, usimamizi duni wa matumizi ya fedha na baadhi ya Halmashauri kushindwa kupata ruzuku ya maendeleo,” alisema.
 
Akizungumzia kuhusu ukusanyaji mdogo wa mapato, Waziri Mkuu alisema uko chini licha ya Halmashauri nyingi kuonesha kuwa zingekusanya mapato na kuongeza vyanzo vya mapato.
 
Reviewed by crispaseve on 11:31 Rating: 5

No comments

Post AD