Header AD

KALAPINA NA CHID BENZ BIFU MWISHO.

 

WAKATI maadhimisho ya miaka 13 ya Kikosi cha Mizinga inatarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa New Msasani Club, kiongozi wa kundi hilo, Karama Masoud 'Kalapina' amefichua kumaliza 'bifu' lake na Chid Benz na kumtangaza kwamba ni miongoni mwa wasanii watakaonegesha onyesho hilo kabambe.
Aidha Kalapina amesema kuwa makundi na msanii yeyote ambaye angependa kujitokeza kushiriki katika show yao hata kama siyo kwa kupanda jukwaani anawakaribisha kwa nia ya kufanikisha maadhimisho hayo na pia kutangaza Amani na Upendo Tanzania.
Akizungumza mapema asubuhi hii, Kalapina alisema Chid Benz naye atakuwepo katika show yao, licha ya kwamba mapema mwezi uliiopita walitibuana baada ya Benz kuvamia shoo ya Kikosi na kulazimika kutimuliwa jukwaani kitemi na kuibua hisia kwamba 'vita' ya wawili hao imeanza.
Hata hivyo, Kalapina alisema kwa sasa kikosi wamekuwa na hivuo wamezika tofauti zao za zamani na kuamua kufanya kazi baada ya kutumia muda mwingi kufanya harakati za kuisimamisha hop hop Bongo ambapo ilikuwa ikipata vikwazo vingi kiasi cha kutotangazika licha ya msaada mkubwa kwa jamii.

"Tumeshakuwa, mambo ya ubabe na kila lililokuwa likiwaudhi watu kwa sasa bhaaas, ndiyo maana Chid mdogo wangu nimemualika na pia naruhusu makundi yote yanayotuunga mkono na wasanii wengine waje ukumbini kutuopa sapoti kwa nia ya kutangaza amani na upendo kupitia tamasha hili la leo," alisema.
Kikosi cha Mizinga kitafanya onyesho hili likisindikizwa na wasanii kibao nyota nchini akiwemo 'Dume la Simba' Afande Sele, Manzese Crew, gangwe Mob, Mansu-Lee, Stereo, Nikki Mbishi, Young Killer na wengine huku kukiwa na maonyesho mbalimbali yenye utamaduni wa hip hop kama uchoraji kudance na mengine kibao.
Reviewed by crispaseve on 02:37 Rating: 5

No comments

Post AD