MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM APIGWA RISASI YA TUMBO NA WATU WANAODHANIWA NI MAJAMBAZI.
Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa
wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo
cha Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya
Yombo chuoni hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho
wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta
wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za
fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi
hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha, na majambazi
kuanza safari yao.Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala
(Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na
kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi
alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa
Hospitalini.Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho
waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao
Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo
walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa mwanafunzi
huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna
taarifa yoyote iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia
suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.
Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es
salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya
kikatili chuoni hapo. Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa
umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini
kinaendelea.
Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani katika
shule za Chuo hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa
komputa zao mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya
uandishi wa Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC).
Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.
Reviewed by crispaseve
on
13:17
Rating:
Post a Comment