Header AD

Umoja wa Watanzania Ujerumani (U.T.U ) Kushiriki katika Festival ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg " Ujerumani litakaloanza Julai 19 hadi 21, 2013

Mhe. Mfundo, Mwenyekiti wa UTU.
Watayarishaji wa Festival ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg, nchini Ujerumani wameuhalika Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushiriki katika maonyesho hayo utamaduni wa nchi mbali mbali yatakayoanza 19 hadi 21 Julai 2013.

Watayarishaji wa maonyesho hayo wamevutiwa sana na shughuli za Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kwa juhudi zake za kuitangaza Tanzania.

Wandaaji hao, wametoa nafasi kwa umoja wa watanzania kushiriki na kuitangaza Tanzania kwa kasi zaidi.

Mwenyekiti wa UTU, Bw. Mfundo Peter Mfundo ameupokea mwaliko huo kwa mikono miwili na amewaomba Watanzania wote wanaoishi Ujerumani kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kuitumia nafasi waliyopewa kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania ambapo Umoja wa Watanzania (UTU) utakuwa na banda lake katika maonyesho hayo.

Mnakaribishwa wote na kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com pia unaweza kutembelea link ya maonyesho at http://www.bruederschaft-der-voelker.de/2013/05/29/union-of-tanzanians-in-germany/
Reviewed by crispaseve on 05:00 Rating: 5

No comments

Post AD