VIDEO NYINGINE IMETOKA INAYOWAONYESHA WANAJESHI WA KENYA(KDF) WAKIIBA SIMU KATIKA DUKA LA SAMSUNG WESTGATE MALL.

Baada ya kamera za CCTV ambazo zilizofungwa Westgate Mall kuwaonyesha wanajeshi wa Kenya(KDF) wakijibebea bidhaa mbalimbali kwenye supermarket ya Nakumatii, video nyingine mpya imetoka inayowaonyesha wanajeshi hao wakiwa katika duka la Samsung wakichukua simu zilizokuwa zinauzwa dukani hapo kama vile zao.
Tukio hilo linakuwa ni muendelezo wa matukio yaliyorekodiwa katika kamera maalum za CCTV wakati wa mapambano na wanamgambo wa Al shabab waliovamia katika maduka hayo mwezi Septemba mwaka jana.
Katika video hiyo inawaonyesha wanajeshi wanne wakiwa wanachukua bidhaa aina ya simu katika duka la Samsung huku wakipasiana na mwengine akionekana akiwa ameinamia eneo la kaunta ndani ya duka hilo.
Wiki mbili zilizopita jeshi la KDF lilitoa taarifa kwamba hakuna wizi wa mali au bidhaa uliofanywa na wanajeshi wao waliokuwa kwenye doria ndani ya jengo la Westgate wakati wa mapambano na wanamgambo wa Al Shabab, huku wakidai kwamba zile video za mwanzo zilizokuwa zinawaonyesha wanajeshi wao wakibeba vitu kwa kudai kwamba yalikuwa ni maji ya kunywa na sio vinginevyo. Tazama VIDEO hiyo hapa chini.
VIDEO NYINGINE IMETOKA INAYOWAONYESHA WANAJESHI WA KENYA(KDF) WAKIIBA SIMU KATIKA DUKA LA SAMSUNG WESTGATE MALL.
Reviewed by crispaseve
on
13:18
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
13:18
Rating:

Post a Comment