MSAMBAZAJI BORA WA BIA ZA TBL AZAWADIWA BAJAJ.
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Kusini, James Bokela (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Massawe Glosary, Jacob Massawe (wa pili kulia) na mkewe Anna Massawe baada ya kuwakabidhi zawadi ya Bajaj yenye thamani ya sh. mil. 4.7, baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa kanda hiyo kwa usambazaji na uuzaji wa bidhaa za TBL. Hafla hiyo ilifanyika Kibaha, Pwani juzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Massawe Glosary, Jacob Massawe (wa pili kulia) na mkewe Anna Massawe (kulia), wakifurahia zawadi ya Bajaj yenye thamani ya sh. mil. 4.7, kwa kugongeana chupa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na wamiliki wa baa wilayani Kibaha, waliyokabidhiwa na TBL, baada ya kampuni yao kuwa washindi wa kwanza Kanda ya Kusini kwa usambazaji na uuzaji bora wa bidhaa za TBL. Hafla hiyo ilifanyika Kibaha, mkoani Pwani.

Post a Comment