TANZANIA YASHINDA VIVUTIO VITATU MAAJABU SABA YA ASILI AFRIKA, NI MLIMA KILIMANJARO, NGORONGORO CRATES NA MBUGA YA SERENGETI
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga
makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa
TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya
Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu
saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto
ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders Bw.
Philip Imler.
Tanzania imefanikiwa kushinda
kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro,
Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo
imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi,
Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika
ukanda wa Afrika Mashariki
Katika picha kulia ni Waziri wa
Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmoja wa
wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates muanzilishi na
muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara
baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya asili ya
Afrika iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini
Arusha.
Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kamavinavyoonekana.
Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB
Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini
Mchungaji Msigwa, Kushoto ni Mh Shah kutoka Mafia na mmoja wa wajumbe wa
bodi ya Utalii TTB
Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzaniaakiwa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria pia.
Mbunge Mh. James Lembeli akisalimiana na Bw. Mike Teyrol walipokutana katika hafla hiyo.
Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya
Utalii Bi Devitha Mdachi akiwa pamoja na maafisa wengine wa bodi hiyo
wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.
Waziri wa
Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza jambo na
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.
Waziri wa
Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi katikati ni msaidizi wake Bw.
Miskanji.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja
na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural
Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia ni Magesa Mulongo mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda
na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural
Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Mkurugenzi wa Hifadhi za taifa
TANAPA Bw. Allan Kijazi akiwasikiliza wabunge waliohudhuria katika hafla
hiyo kulia ni Deo Filikunjombe na kushoto ni David Kafulila.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki wakati
alipowasili kwenye hoteli ya Maount Meru kwa ajili ya utoaji tuzo hizo.
Mama Tunu Pinda wa pili kutoka
kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler kutoka Seven
Natural Wonders.
Mabalozi mbalimbali waliohudhuria
katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Mutinda Mutiso Balozi
wa Kenya Nchini Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini
Bw. Godbless Lema kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla hiyo.
Bw Allan Kijazi kushpto akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates Mkurugenzi wa Hifadhi
za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi katika hafla hiyo, kushoto ni Philip
Imler wa Seven Natural Wonders.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea katika hafla hiyo.
muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.
Balozi Khamis Kagasheki ambaye pia
ni Waziri wa Maliasili na Utalii akizungumza katika hafla hiyo
iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania
akizungumza na Balozi Charles Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini
Tanzania TTB na Mkurugenzi wa bodi hiyo Dk. Aloyce Nzuki wakati wa hafla
hiyo.
Reviewed by crispaseve
on
03:23
Rating:
Post a Comment