WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI (IAEA) YUKIYA AMANO WAZINDUA JENGO JIPYA JIJINI DAR ES SALAAM LENYE VIFAA VYA KISASA KUSHUGHULIKIA MAGONJWA YA KANSA NCHINI
Waziri mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (katikati) akikata utepe kwa kushirikiana na Mkurugenzi
mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani Yukiya Amano
(wa pili kutoka kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo jipya lenye
vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika
Taasisi ya Kansa Ocean Road jijini Dar es salaam. Wengine ni Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto),
Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kansa Ocen Road Prof. Twalib Ngoma (wa
tatu kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif
Rashid.
Waziri mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (katikati) akiwaonyesha wageni mbalimbali waliohudhuria
uzinduzi wa jengo jipya la kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika
Hospitali ya Kansa Ocean Road kitabu cha Mkakati wa Kitaifa wa
Kudhibiti na kupambana na Kansa nchini.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la
Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani Yukiya Amano akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam mara baada ya
kuzinduliwa kwa jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa
na serikali ya Tanzania huku shirika hilo likitoa msaada wa mashine
mbili kwa za kutambua athari za ugonjwa wa kansa kwenye mwili wa
binadamu.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam
mara baada ya kuzindua jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road
lililojengwa na serikali ya Tanzania lenye uwezo wa kuhudumia wa 257 kwa
gharama ya shilingi bilioni 7.2 huku Shirika la nguvu za Atomiki
Duniani (IAEA) likichangia mashine 2 za kutambua sehemu zilizoathiriwa
na ugonjwa wa kansa katika mwili wa binadamu zenye uwezo wa kuhudumia
wagonjwa 1600 kila moja kwa mwaka.
Baadhi ya wataalam wa Taasisi ya
Kansa ya Ocean Road wakiwa ndani ya moja ya chumba cha jengo jipya
lililozinduliwa jijini Dar es salaam chenye moja ya mashine yenye uwezo
wa kuwahudumia wagonjwa 1600 kwa mwaka. Mashine hiyo imetolewa na
Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).
Sehemu ya nje ya jengo jipya la Taasisi ya Kansa ya Ocean Road lenye vifaa vya kisasa lilozinduliwa jijini Dar es salaam.
Reviewed by crispaseve
on
00:47
Rating:
Post a Comment