Header AD

African Barrick Gold (ABG) yatoa Tuzo kwa Wafanyakazi Bora Migodi ya Bulyanhulu na North Mara

Mfanyanyazi wa Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG), Simon Shayo akiwa na tuzo ya ufanyakazi bora kwenye idara ya mahusiano ya jamii wakati wa sherehe zilizofanyika mgodini hapo Mkoani Mara hivi karibuni.  Shayo na timu nzima ya mgodi huo wamepewa tuzo hiyo kutokana na mradi wa kusaidia kikundi cha wanawake cha Nyabichune kijikwamue kiuchumi.

Makamu wa Rais Mtendaji na Afisa Mwandamizi (Executive Vice President & Chief Operating Officer) wa kampuni ya Barrick Gold Corp,Igor Gonzales  (kushoto), akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa Godfrey Nyabuzoki, mfanyakazi wa kitengo cha ulinzi cha mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold kwenye sherehe iliyofanyika mgodini hapo mkoani Mara hivi karibuni. Godfrey na wafanyakazi wengine watano wa kitengo cha ulinzi cha mgodi huo walionesha ujasiri mkubwa kukabiliana na kundi kubwa la wananchi waliovamia mgodi huo mwezi Machi mwaka huu na wafanyakazi hao wakaweza kumuokoa mwenzao aliyeumia. Kulia ni makamu wa rais wa kampuni ya Barrick Gold Corp. anayeshughulikia masuala ya ulinzi, Mark Wall.

Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold, Lolence Kasekenya (katikati), akiwa na zawadi yake ya mfanyakazi bora kwenye kitengo cha mahusiano ya jamii katika sherehe iliyofanyika kwenye mgodi huo uliopo wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga hivi karibuni. Kulia ni  Makamu wa Rais Mwandamizi wa kampuni ya Barrick anayeshughulikia Usalama na Uongozi, Don Ritz na Mkurugenzi Mwandamizi wa ABG upande wa Mahusiano ya Jamii na Mazingira. Kevin D'Souza.

Afisa Mwandamizi wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold, Marco Zolezzi akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa mfanyakazi wa kitengo cha uchunguzi cha mgodi wa Bulyanhulu, Gilbert Kalisa, kwenye sherehe zilizofanyika kwenye mgodi huo uliopo wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga hivi karibuni.
Reviewed by crispaseve on 16:11 Rating: 5

No comments

Post AD