ALBINUS AWA MFALME WA UZITO WA UNYOYA WA DUNIA KWA VIJANA
Albinu Felesianu wa
Namibia leo ameudhihirishia ulimwengu kuwa yeye kweli ndiye Mfalme wa
uzito wa unyoya duniani kwa vijana baada ya kumgalagaza bondia Herbert
Quartey wa Ghana katika mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa
Windhoek Country Club Resort and Casino leo tarehe 29, March 2013.
Umati wa watu wasiopungua elfu 20
walijazana katika ukumbi huo wa burudani wakimshangilia kwa nderemo na
vifijo bondia wao Albinus wakati alipokuwa anafanya vitu vyake kwenye
ulingo.
Baada ya mtangazaji wa ulingo
kutamka kuwa “Na sasa bingwa mpya wa uzito wa unyoya duniani kwa vijana
ni Albinus Felesianu” mayowe ya wapenzi wa ngumi waliojazana katika
ukumbi huo yaliweza kusikika kilometa tatu mpaka katikati ya jiji la
Windhoek.
Hata hivyo, haikuwa kazi rahisi
kwa Albinus kuunyakua mkanda wa ubingwa wa dunia kwa vijana kwani Mghana
Herbert Quartey naye alikuwa mbogo kwani alirusha kila aina ya masumbwi
yaliyomo kwenye kitabu.
Wawili hao walichapana makonde
mazito kama watu wenye uzito mkubwa na kama sio uwezo na ujuzi wa
referii Deon Dwarte wa Afrika ya Kusini kazi ingekuwa ngumu sana kwani
kila bondia alijaribu kumpata mwenzake katika sehemu zinazoumiza ili
kuumaliza mpambano mapema lakini ujuzi na ubishi wa kila mmoja ulifanya
kusiweko na knockout yoyote!
Hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya
Namibia kuweza kuandaa mpambano wa ubingwa wa dunia wa IBF na wakali
hao waliweza kuufanya umati wote uliohudhuria kulipuka kwa makelele ya
kushangilia kila wakati.
Alikuweko Harry Simon, ambaye
ndiye Mnamibia aliyeweza kuufanya mchezo wa ngumi kupendwa na kuwa
maarufu sana nchini humu. Uwezo na utukutu wa Harry Simon ulingoni
umeufanya mchezo wa ngumi kupendwa karibu na kila Mnamibia.
Walikuweko pia wageni wengine
wengi lakini kampuni ya simu ya Telecom ambayo ndio waliokuwa wadhamini
wa mpambano huo imejikusanya kila aina ya sifa na upendo kutoka kwa
wananchi wa Namibia jinsi inavyo dhamini mchezo wa ngumi!
Mpambano huu uliandaliwa na Kinda
Nangolo wa kampuni ya Kinda Boxing Promotions ambayo ndio waandaaji wa
mpambano ujao wa mwezi wa Mei wa bingwa wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi
na Mashariki ya Kati katika uzito wa unyoya bondia Gottlieb Ndokosho.
Mpambano wa IBF wa Kimataifa wa bondia Harry Simon nao utafanyika mwezi
wa Juni.
Reviewed by crispaseve
on
09:52
Rating:
Post a Comment