HOTELI YA DOUBLE TREE BY HILTON YA JIJINI DAR YAENDELEZA KAMPENI YA MATUMIZI YA TAA ZA NISHATI YA JUA KWA SHULE YA MSINGI MIKOCHENI A
Meneja Mkuu wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Sven Lippinghof aliyeambatana na Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli hiyo Bw. Florenso Kirambata akisaini kitabu cha wageni katika Shule ya Msingi Mikocheni A walipowasili shuleni hapo kuendeleza kampeni ya matumizi ya taa za nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Salehe Makwiro.
Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli hiyo Bw. Florenso Kirambata akitia saini kitabi cha wageni katika shule hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Sven Lippinghof (katikati) na Mkurugenzi
wa Masoko wa Hoteli hiyo Bw. Florenso Kirambata (kulia) kwa pamoja
wakimkabidhi moja ya boksi zenye taa zinazotumia nishati ya Jua Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Mikocheni A Salehe Mwakwiro ikiwa ni muendelezo
wa kampeni ya matumizi ya nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za mkoa wa Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso
Kirambata (kulia) akitoa somo ya matumizi ya taa zinazotumia nishati ya
Jua ambazo pia ni rafiki wa mazingira kwa Wanafunzi wa darasa la Saba wa
Shule ya Msingi Mikocheni A na kuwaasa kuepeuka kutumia vibatari muda
wa kujitosema ambavyo vimekuwa vikisababisha majanga ya kuungua kwa
watoto wengi nchini. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bw. Sven Lippinghof.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mikocheni
A wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by
Hilton Florenso Kirambata (hayupo pichani) wakati akiwapa somo la
matumizi ya taa zinazotumia Nishati ya Jua ambazo pia ni rafiki wa
Mazingira.
Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso
Kirambata akitoa maelekezo jinsi ya kutumia taa hizo kwa wanafunzi wa
darasa la saba wa shule hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli hiyo Bw. Florenso Kirambata
akiwaonyesha mwanga wa taa hizo za nishati ya Jua ambazo ni imara na
zinadumu kwa muda wa miaka 10 na zenye uwezo wa kutumika masaa 4 mpaka
kuisha chaji yake.
Wanafunzi wa Darasa la Saba katika
shule msingi Mikocheni A wakati wa hafla ya kukabidhiwa taa zinazotumia
Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton.
Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo zitawasaidia
kujisomea hata kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani hivyo kuongeza
uwezo wao kielimu.
Kampeni hiyo Hoteli ya DoubleTree by
Hilton itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua
kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo
likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme
ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.
Reviewed by crispaseve
on
16:06
Rating:
Post a Comment