Header AD

BREAKING NEEEEEWZ.MBUNGE WA ARUSHA GODBLESS LEMA AACHIWA KWA DHAMANA

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema, leo amepandishwa kizimbani jijini Arusha na kusomewa shitaka lililokuwa likimkabili na kuachiwa kwa dhamana iliyokuwa na masharti rahisi.

Godless Lema,  alikuwa akishikiliwa na polisi mkoani humo kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu zilizosababishwa na wanafunzi kwenye chuo cha Uhasibu mwanzoni mwa wiki iliyopita mwenzao kuuwawa huko maeneo ya njiro jijini humo.

Mbunge huyo alikamatwa siku ya Ijumaa na kuwekwa rumande kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha, Magesa Mulongo.

Baada ya kuachiwa mahakamani hapo mbunge huyo ameongozana na wafuasi wake kwa msafara wa maandamano na mapikipiki kuelekea katika Ofisi za Chama hicho.
Reviewed by crispaseve on 09:45 Rating: 5

No comments

Post AD