Rais Kikwete akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge Corporation MCC ikulu jijini Dar leo,Pia apongeza walioshiriki Zoeazi la Uokozi Ajali ya Jengo la Ghorofa Dar
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge
Corporation MCC Bwana Daniel Yohannes ikulu jijini Dar es Salaam
leo.Kushoto ni Balozi wa Marekani Alfonso Lenhardt.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akioongea na makundi mbalimbali pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama
vilivyoshiriki katika zoezi la uokozi wakati wa ajali ambapo jengo la
ghorofa liliporomoka , kuuwa na kujeruhi watu kadhaa katikati ya Jiji la
Dar es Salaam hivi karibun.Hafla hiyo fupi ilifanyika katika ukumbi wa
Sabasaba katik viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Sabasaba Barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar
es Salaam,Suleiman Kova kwa uendeshaji wa Zoezi la uokoaji katika ajali
ya Jengo lililoporomoka jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na kijana mlemavu Shabani Selemani Mohamed katika ukumbi
Sabasaba katuka viwanja vya maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa
,wakati wa hafla fupi ya kupongeza makundi mbalimbali yaliyoshiri katika
kazi ya kuokoa watu na kuopoa miili wakati wa ajali ya kuanguka kwa
ghorofa katikati ya Jiji la Dar e Salaam hivi karibuni.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete akiwapongeza baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ
walishiriki katika kazi ya kuokoa watu wakati wa ajali ya kupomoka kwa
jengo katikati ya jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.picha na Freddy
Maro

Post a Comment