Header AD

BALIMI YAENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI MKOANI TABORA

Mgeni rasmi katika mashindano ya ngoma za asili kwa Mkoa wa Tabora Mstahiki Meya wa manispaa ya Tabora Gulamhussein Remtullah akizungumza na wakazi wa Mkoa huo katika mashindano hayo chini ya udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Balimi Extra , mashindano hayo yamefanyika katika shule ya sekondari Iyungi.tolle
 Kushoto meneja wa matukio wa kampuni ya Bia Tanzania - tbl kanda ya ziwa  Bwana Erick Mwayela akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Tabora Mstahiki Meya Gulamhussein Remtullah kitita cha shilingi laki sita ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya Ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia aliyevaa fulani ya balimi ni kiongozi wa kundi la Mwenge la manispaa hiyo ambao ndio wameibuka washindi wa shindano hilo.
Meya wa Manispaa ya Tabora katikati Akimkabidhi kiongozi wa kundi la Mwenge fedha tasilimu shilingi laki sita mara baada ya kundi hilo kutangazwa Washindi wa shindano la ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora ambalo limefadhiriwa na kampuni ya Bia Tanzania Tbl kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia kwake ni Meneja matukio wa kampuni hiyo kanda ya Ziwa Bw Eric Mwayela.

HATIMAYE FAINALI ZA MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI KWA MKOA WA TABORA AMBAYO YAMEDHAMINIWA NA KAMPUNI YA BIA TANZANIA-TBL KUPITIA BIA YAKE YA BALIMI EXTRA YAMEMALIZIKA RASMI KWA KUNDI LA MWENGE KUIBUKA BINGWA WA MASHINDANO HAYO NA KUJINYAKULIA KITITA CHA SHILINGI LAKI 6 NA HIVYO KUPATA TIKETI YA KUUWAKILISHA MKOA HUO KATIKA MASHINDANO YA KANDA YATAKAYO FANYIKA JIJINI MWANZA HIVI KARIBUNI.

KATIKA KINYANG'ANYILO HICHO AMBACHO KIMEVUTA HISIA ZA WAKAZI WENGI WA MKOA HUO, KUNDI HILO LIMEIBUKA MSHINDI KWA ALAMA 90 LIKIFUATIWA NA KUNDI LA MAGEREZA AMBAYO IMEPATA ALAMA 87 NA KUONDOKA NA ZAWADI YA SHILINGI LAKI 5 HUKU NAFASI YA TATU IKICHUKULIWA NA MASANGE JKT AMBAO WAMEJINYAKULIA SHILINGI LAKI 400 KWA KUPATA ALAMA 77, NAFASI YA 4 IMECHUKULIWA NA KUNDI LA MWAMKO SIKONGE NA KUJIPATIA SHILINGI LAKI 3KWA KUPATA ALAMA 63.

KATIKA MPAMBANO HUO AMBAO UMEVISHIRIKISHA VIKUNDI 10 WASHIRIKI WOTE KUANZIA NAFASI YA 5 MPAKA YA 10 WAMEJINYAKULIA ZAWADI YA FEDHA TASILIMU SHILINGI LAKI MOJA NA NUSU HUKU MEYA WA MANISPAA HIYO MSTAHIKI MEYA GULAMHUSSEIN REMTULLAH AMBAYE NDIYE ALIYE KUWA MGENI RASMI AKIIPONGEZA KAMPUNI HIYO KWA KUDHAMINI MASHINDANO HAYO AMBAPO KUPITIA MASHINDANO HAYO JAMII IMEKUWA IKIJIKUMBUSHA TAMADUNI ZETU.

GULAMHUSSEIN AMESEMA KUTOKANA NA KAMPUNI HIYO KUFANYA MASHINDANO HAYO KATIKA KIPINDI HIKI CHA MAVUNO HII INADHIRISHA KWAMBA BIA HIYO YA BALIMI EXTRA INAMJALI NA KUMSAMINI MKULIMA WA KITANZANIA.

AIDHA MEYA HUYO AMELITAKA KUNDU HILO LA MWENGE KWENDA KUUWAKILISHA VYEMA MKOA WA TABORA NA KUHAKIKISHA KUWA WANALEJEA NA USHINDI KATIKA MASHINDANO YA KANDA AMBAYO YANATALAJIA KUFANYIKA JIJINI MWANZA HIVI KARIBUNI.

AWALI MENEJA WA MATUKIO WA KANDA YA ZIWA BWANA ERICK MWAYELA AMESEMA KUWA KAMPUNI YAKE KUPITIA BIA YA BALIMI EXTRA WANAJISIKIA FAHARI KUDHAMINI MASHINDANO HAYO AMBAPO AMEFAFANUA KUWA KUPITIA MASHINDANO HAYO WATU WAMEKUWA WAKIFAHAMIANA NA KUKUMBUKA NGOMA ZA ASILI ZA MAKABILA YETU.

MASHINDANO MENGINE KAMA HAYO YANATALAJIWA KUFANYIKA MJINI SHINYANGA MWISHONI MWA WIKI IJAYO AMBAPO VIKUNDI MBALIMBALI VYA MKOA HUWA VITAPATA FULSA YA KUSHIRIKI KATIKA MPAMBANO HUO NA HIVYO KUWATAKA WAKAZI WA MKOA HUO KUJITOKEZA KWA WINGI ILI KUSHUHUDIA MWAKILISHI WAO KATIKA MASHINDANO YA KANDA.
Reviewed by crispaseve on 03:17 Rating: 5

No comments

Post AD