HEKA HEKA: MWANAMAMA ASHINDA JUU YA PAA SIKU TANO KUZUIA NYUMBA YAKE ISIPIGWE MNADA NA BENKI.
Huyu mama alikaa juu ya paa kwa siku
tatu tangu jumamosi kupinga nyumba yao kuchukuliwa na bank.Anasema
mumewe alimdhamini mtu alipochukua mkopo bank miaka mingi iliyopita na
kushindwa kulipa mkopo huo.
Kwa mujibu wa maelezo yake kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali zake zilizotaifishwa.
Mdaiwa alikopa ml 240 wameuza nyumba zake 2 na mabasi
mawili.Wenyewe wanachodai katika hilo deni imebaki tsh ngapi na wao
watoe?kama nyumba iuzwe watoe deni la bank na hela inayobaki wabaki nayo
wao.
Nyumba ipo mbezi Tangi bovu na inaeneo
kubwa sana mama anasema hata akiuza si chini ya ml 500 iweje atolewe
kwa ml 240?wakati mdaiwa nyumba zake mbili zimeshachukuliwa na mabasi
mawili yale makubwa ya safari za mikoani.Hiyo ml 240 haijatimia tu?na
kama bado kiasi gani kimebaki?
Ndani ya nyumba vitu walishachukua hao
watu wa auction mart ndani kweupe.Na wakati haya yakiendelea hakukuwa
na amri yoyote iliyotoka mahakamani wala hawakuwa na kibali cha
mahakama.
Gea alimfata huko huko juu kumsikiliza na tumemsikia leo kwenye heka heka.Kesho pia itaendelea…
Chumba cha habari cha clouds fm kimeenda kufatilia hapo bank ya Tanzania Investment bank(TIB)kujua kulikoni??
Maana wakati haya yakiendelea hiyo jana inasemekana hii nyumba
imeshauzwa.Inauzwaje na shauri lipo mahakamani?Na jana mume wa huyu mama
alikuwa mahakamani maana ilikuwa siku ya kesi kuendelea kusikilizwa.
Reviewed by crispaseve
on
10:58
Rating:
Post a Comment