Marieta atwaa taji la Redd’s Miss Chang’ombe.
Na Mwandishi Wetu
MREMBO
Marieta Boniface juzi usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss
Chang’ombe, katika kinyang’anyiro kilichokuwa kikali kilichofanyika
kwenye viwanja vya TCC Club, vilivyopo Chang’ombe, Dar es Salaam.
Marieta alifanikiwa kuwashinda warembo wengine 12 walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho ambacho kilikuwa na upinzani mkali.
Kutokana
na ushindi huo, Marieta alizawadiwa pikipiki yenye thamani ya Sh
milioni 1.5 ambayo ilitolewa na wadhamini wenza Kampuni ya Kishen
Enterprises Ltd.
Mbunge
wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu aliyekuwa mgeni rasmi ndiye
aliyemkabidhi zawadi hiyo na kusema amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na
shindano hilo na yupo tayari kulisaidia zaidi.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa taji, Marieta alisema anaamini kwa dhati
atafanikiwa kufika mbali zaidi kwani amedhamiria kuhakikisha anaibeba
Chang’ombe katika shindano la Redd’s Miss Tanzania.
Shindano
la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

Post a Comment