DUDE JIPYA LA FARID KUBANDA (FID Q) SIRI YA MCHEZO LYRICS
Verse 1
Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na umuhimu kihivyo…
stimu zikanipa elimu ya Biko/ Kimaandiko… kimistari.. hadi fans
wanascream nikirap../ sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream
hiphop/ Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/ Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa #teamMabiiitoz / Achana na power window.. sijui rimz za dimpoz/ haileti bingo, mshiko? Star ishi simple/ sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/ wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/ jikombe ugongwe…mtaaa ukuone hauna ishu/ ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/ Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za harakati ni ujinga?/
HAPANA…. nguvu ya mamba ni maji/ na umaarufu au kutamba.. kushika
namba ni bahati..sio kipaji kama Kubanda eti unachana kigumu/ kisa
track ikivuma sana kwenye chati haidumu / Amani kwa chachage na
MAKUWADI wa SOKO HURIA../ baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI
ya BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../ najiuliza
tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na
wakinitisha najihami../ inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni
jirani/ ‘’Pole MAPROSOO’’ ( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu.. / WAZEE ni wahuni hadi soo waay back before SUGU/
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu/ na MBWA MWITU wenye
siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../
huo ni utumwa pia/Unafanya vijana wanaumia../ Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia..
CHORUS: ( Juma Nature )
Siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza.. kisha utapata/ x 2 Siri ya mchezo naijua mimi.. tu.. na hakuna mwingine x 2
VERSE 2:
Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara inaweza buma/ wakati SIASA
kila mara ukiwa unang’ara ujue kuna.. kinara/ anayeunda msafara wa
wanaojituma na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna/
KIDUMU CHAMA CHA MASELA… Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,/ tuone kufuru za wenye hela/
TANZANIA ni ‘ demu wa mtungo ‘ wanamuiita CHA WOOTE/’’ HANGOVER ..
‘’anaikimbia kwa kupiga ‘ “ mtungi “ saa zote /Mkubwa anazuga atasolve…
matatizo ya nchi yake/ ‘’na gari bovu..’’ halisukumwi kwa kukaa ndani
yake/ MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza../ je Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza? / hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion/ na daily tunafeli sababu ya POLITICAL institutions/ CIVILIZATION imeadvance sasa wanatuua economically../ hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free/ Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu/ kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/ Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua..? zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua? Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka/ Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA/ Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua nani leo atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????
Post a Comment