MAAJABU: Kontena lakutwa na shehena la Vikarogosi pamoja na viungo vya Binadamu kutoka china Vikisadikiwa ni vya dini za Masheteni

Wengi walioipata hii taarifa wanashangaa imekuaje ni viungo tu vya
binadamu vimepatikana kwenye kontena zima vikiwa vinaingizwa Kenya?
vinakwenda wapi? kazi yake ni nini?
Taarifa iliyoripotiwa na Citizen TV Kenya inasema Shehena hii
iliyokamatwa baada ya kupitishwa kwenye bandari ya Mombasa inasemekana
imesafirishwa na Mwanasiasa maarufu ambae kabla ya kukamatwa alisema
ilikua na bidhaa za nyumbani ambapo ilipofika kwenye kituo cha ukaguzi
wa mashehena cha Changamwe ilipatikana na vikaragosi vya mafuvu na
mifupa ya binadamu ndipo amri ikatoka kontena likamatwe.
Baadhi ya mifupa ya binadamu iliyopatikana ni pamoja na mafuvu, miguu
na mikono pamoja bidhaa za nyumba ambapo vyote kwa pamoja vilikua
vinasafirishwa ambapo Afisa wa maswala ya Uhusiano mwema wa KRA Fatuma
Yusuf alithibitisha kwamba hii shehena iliingia kutoka China siku ya
pili ya October 2013 kabla ya kugundulika ilikua na vikaragosi vya
kutisha ikiwemo mifupa ya binadamu.
Mpaka
sasa uchunguzi wa shehena hili unaendelea lakini baadhi ya wakazi wa
Mombasa wameonyesha wasiwasi wao na kusema kuna haja ya Serikali kutoa
ripoti ya ibada za kishetani ambayo inasemekana kubuniwa na Rais Mstaafu
Daniel Arap Moi miaka kadhaa iliyopita.















Post a Comment