Majina ya vyuo 9 vilivyofutwa na Serikali kwa kukosa sifa
Serikali kupitia Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi imevifuta vyuo ambavyo havina sifa ikiwamo kukosa
usajili wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na kufundishwa na
walimu wasio na sifa. Vyuo vilivyotangazwa kufutwa ni:-1. Media and Values Training Institute (Dar es Salaam)2. Information Technology Training Center (Dar es Salaam)3. Dar es Salaam School of Hair Design (Dar es Salaam)4. Morogoro School of Medical Sciences (Morogoro)5. Media and Research Center6. Vision Hotel and Tourism College7. East Africa College of Hospitality and Tourism8. The Africa Institute of Business Management9. Aspiration Training Center (P.T)
Naibu Waziri wa Wizara husika , Philip
Mulugo, alitangaza hatua hiyo wakati alipokutana na Kamati ya Bunge ya
Huduma za Jamii, katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Profesa Sifuni Mchome, alisema Serikali ilishatangaza kuwa vyuo visivyo
na sifa vifungwe lakini tatizo likawa ni jinsi ya kuwatafutia wanafunzi
waliopo vyuo vingine. Source: http://www.wavuti.com
Post a Comment