Mbunge wa Jimbo la Songea
Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(watatu kushoto) akiwa na Watendaji wa Halmashauri
ya Manispaa ya Songea, Madiwani na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilayani
humo wakati walipokuwa wanakagua ujenzi wa maabara, mabweni pamoja na
nyumba za walimu wa Shule ya Sekondari ya Mdandamo iliyopo katika Kata
ya Mletele, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Dk Nchimbi yupo mjini
Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali
ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Mbunge wa Jimbo la Songea
Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(aliyevaa mawani) akiwa na Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Madiwani na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
wilayani humo wakilikagua daraja lililopo katika Kata ya Mletele ambalo
lipo hatua ya mwisho kukamilika. Hata hivyo, Dk Nchimbi alichangia Shilingi
milioni moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa daraja hilo. Dk Nchimbi
yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua
miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Mbunge wa Jimbo la Songea
Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akikagua ujenzi wa maabara ya kisasa ya
Sekondari ya Mdandamo iliyopo katika Kata ya Mletele, Manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Joseph Mkirikiti.
Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja
na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Msanii maarufu wa kuigiza sauti mbalimbali za Viongozi wa Serikali,
wanasisa, watangazaji wa habari za kwenye Luninga na redio, pamoja na
wasanii mbalimbali nchini, Adamu kwa jina maarufu ‘Mlugaluga’ akitoa
burudani kwa wananchi wa Mtaa wa Liwumbu, Kata ya Mletele, Manispaa
ya Songea kabla ya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kulia) kuzungumza na
wananchi hao kuhusiana na masuala mbalimbali ya maendeleo ya kata hiyo.
Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja
na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na mamia
ya wananchi wa Kata ya Matarawe, Mjini Songea kuhusiana na masuala mbalimbali
ya maendeleo ya kata hiyo, hata hivyo Dk Nchimbi aliwahakikishia wananchi
wake kuwa, kwa kushirikiana na Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa
ya Songea watalitengeza Daraja la Matarawe ambalo mara kwa mara linasababisha
ajali mbalimbali zikiwemo za bodaboda. Dk Nchimbi yupo mjini Songea
kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali
ya maendeleo iliyopo jimboni mwake. Picha zote na Felix Mwagara.
Reviewed by crispaseve
on
21:47
Rating:
Post a Comment