KALAMA NYILAWILA ASAINI MKATABA WA KUCHEZA NA BINGWA KATI YA MASHALI AU KASEBA MEI MOSI
| Promota wa ngumi nchini Ali Mwazoa akipeana mkono na Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi baada ya kumsainisha bondia Kalama Nyilawila katikati anaetarajia kuzipiga mei mosi. |
| Promota
wa ngumi nchini Ali Mwazoa akipeana mkono na Rais wa TPBO Yassin
Abdallah 'Ostadhi baada ya kumsainisha bondia Kalama Nyilawila katikati
anaetarajia kuzipiga mei mosi Picha na www.superdboxingcoach. |
========== ========= =======
Bondia
Kalama Nyilawila ameingia mkataba wa makubaliano na promota Ali Mwazoa
wa Tanga kwa ajili ya mpambano wa Mei Mosi mwaka huu ambapo anasubiri
mshindi wa mpambano kati ya Thomasi Mashali na Japhert Kaseba ambao
watazichapa March 29 katika ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo mshindi
atacheza na
Akizungumza
baada ya kusaini mkataba huo bondia Kalama Nyilawila alijitapa kwa
kusema iwe Mashali awe Kaseba yoyote atakae kutana nae ato kuwa na
masihara nae atampiga kipigo cha mbwa mwizi kwani nafasi hiyo alikuwa
anaitafuta siku nyingi baada ya kupoteza huwezo wake katika masumbwi
hivyo sasa wakae mbali na mimi kwani nakuja kwa nguvu mpya kabisa
akisema atakuwa hatari kama 'Mbeya City' timu ambayo inatoka mkoani kwao
na kufanya maajabu kwa kuitawala ligi kuu ya Tanzania bara ndivyo na
mimi nitakavyofanya
Kalama
katika harakati zake za kuhakikisha anarudi katika chati kama zamani
mechi yake ya mwisho katika kuukaribisha mwaka 2014 alimsambalatisha
bondia Ibrahimu Maokola bila huruma kwa kumpiga K,o ya raundi ya pili
mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Msasani klabu
Nae
promota wa mpambano huo Mwazoa amesema kila kitu kinaendelea vizuri
ikiwemo mapambano ya utangulizi yenye mabondia bora wanaotamba kwa sasa
ambao wapo kwenye kiwango cha ali ya juu kwa kuwa mwaka huu ni wa
masumbwi nchini Tanzania nimeanza na nitaendelea kusapoti na kupromot
mchezo wa ngumi popote nchini
akizungumza
kwa niaba ya chama kilichopewa dhamana ya kusimamia mchezo huo wa mei
mosi Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ostadhi' amesema watanzania wana
bahati sana kwa kujitokeza promota mwenye uchu wa maendeleo kwa mabondia
kwana mabondia wote wame saini mkataba na kupewa posho ya kufanyia
mazoezi isipokuwa bondia mmoja tu kati ya watakaocheza march 29 ni
Kaseba au Mashali jibu ndio tunasubili siku hiyo nani zaidi na
atakaepata nafasi ya kuchapana na Kalama
KALAMA NYILAWILA ASAINI MKATABA WA KUCHEZA NA BINGWA KATI YA MASHALI AU KASEBA MEI MOSI
Reviewed by crispaseve
on
08:28
Rating:

Post a Comment