WAJASILIAMALI KUPATIWA MAFUNZO IRINGA
Fredrick Mwakalebela mmoja wa wakufunzi watakaotoa mafunzo kwa wajasiliamali wa mkoa wa Iringa Feb 22
Mratibu
wa semina ya ujasiliamali Anzawe Chaula akizungumza kuhusu semina hiyo
ya februari 22 ofisini kwake. (Picha na Denis Mlowe)
======== ======= =========
WAJASILIAMALI KUPATIWA MAFUNZO IRINGA
Na Denis Mlowe,Iringa
KAMPUNI
ya Vannedrick Tanzania limited (VTL) ya jijini Dar salaam kwa
kushirikiana na Kituo cha Maendeleo,Haki na Utetezi TCDA cha mjini
Iringa wameandaa semina ya ujasiliamali kwa wakazi wa manispaa ya Iringa
zaidi 1000 inayotarajiwa kufanyika Februari 22 mwaka huu.
Akizungumza
mratibu wa Semina kutoka TCDA Anzawe Chaula alisema lengo la kuandaa
semina hiyo itakayojulikana kwa jina la Jukwaa la Wajasiliamali ni
kuwakomboa wakazi wa mkoa wa Iringa kuondokana na umaskini na kuweza
kujitambua katika utengenezaji wa malighafi mbalimbali.
Alisema
katika semina hiyo itafanyika katika ukumbi wa Hallfare kutakuwa na
mafunzo mbalimbali yanayohusu elimu juu ya kutafuta masoko ya bidhaa kwa
wajasiriamali, jinsi ya kupata fursa za mikopo kutoka katika benki
mbalimbali za ndani nan je ya nchi ya Tanzania.
Chaula
alisema jukwaa la wajasiliamali litawafundisha wajasiliamali kutambua
haki za kisheria katika biashara wafanyazo pamoja na kuratibu mafunzo ya
mara kwa mara ya kuwajengea uwezo katika shughuli zao za kila siku.
“Kuna
umuhimu mkubwa sana kwa wajasiliamali kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara
katika shughuli zao wazifanyazo kutokana na wengi wao kufanya biashara
bila kuwa na elimu mtambuka ya kufanya kazi hizo na kuweza kujiongezea
vipato hivyo sisi tutawapatia mafunzo hayo na naomba sana wajitokeze kwa
wingi kuweza kuelimika juu ya ujasiliamali.” Alisema Chaula.
Aliongeza
kuwa semina hiyo itawajengea uwezo wajasiliamali katika kutafuta na
kutambua fursa mbalimbali zilizoko katika mkoa wa Iringa zikiwemo za
utalii wa ndani ambao uko chini sana katika kutumia fursa hizo.
Aidha
wajasilimali watapatiwa fursa ya kufungua biashara zinazoendana na
wakati uliopo ukiwemo ujenzi wa barabara ya Iringa hadi Dodoma
inayotarajiwa kukamilika mwakani kuweza kufungua miradi mbalimbali
pembezoni mwa barabara hiyo na kuwatumia wanafunzi walioko vyuoni
kujiongezea mapato.
Chaula
alisema katika semina hiyo wakufunzi watakaoelimisha wajasiliamali ni
Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF), Dk Didas Lunyungu kutoka Dar salaam na
Fredrick Mwakalebela na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi.
WAJASILIAMALI KUPATIWA MAFUNZO IRINGA
Reviewed by crispaseve
on
09:28
Rating:

Post a Comment