PICHA KUTOKA KAMPENI ZA CCM KALENGA:JIONEE MWENYEWE JINSI KAMPENI ZA CCM ZILIVYOTUA KIJIJINI IKUVILO KWA MGOMBEA WA CHADEMA LEO
Mwenyekiti wa Chadema katika kijiji cha Wangama jimbo la Kalenga,
Iringa Vijijini, Fred Mgata (kulia) akikabidhi kadi ya chama hicho kwa
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, baada ya kutangaza kuhamia
CCM, kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa CCM jimboni humo,
leo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wapo wanachama wengine 50
alioambatana nao kutoka Chadema. Kijiji hicho cha Wangama ndiko
anakotoka mgombea wa Chadema katika uchaguzi huo, Grace Tendega.
Mwanamke, mkazi wa Kijiji cha Wangama akimpongeza Fred Mgata baada ya uamizi wake wa kuhamia CCM kutoka Chadema.
Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Seif Shabani Mohammed
akihutubia mkutano wa kampeni za CCM katika kijiji cha Ikuvilo, jimbo la
Kalenga leo.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Arusha Mjini, Rehema Mohamed
akisisitiza jambo alipohutubia mkutano wa kampeni za CCM katika jimbo la
Kalenga, leo.
Kada wa CCM kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, Juliana
Shonza akisalimia wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika
leo, Kijiji cha Ikuvilo.
Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa akiwashukuru kina mama baada ya mkutano wake wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Wangama leo.
Mgombea wa CCM jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akimshukuru
Mwenyekiti wa Chadema Kijiji cha Wangama baada ya kutangaza kuhamia CCM
leo.
Wananchi
wsa Kijiji cha Wangama wakiishangilia CCM kwenye mkutano wake wa
kampeni uliofanyika katika kijiji hicho leo.Picha na Bashir Nkromo
PICHA KUTOKA KAMPENI ZA CCM KALENGA:JIONEE MWENYEWE JINSI KAMPENI ZA CCM ZILIVYOTUA KIJIJINI IKUVILO KWA MGOMBEA WA CHADEMA LEO
Reviewed by crispaseve
on
22:19
Rating:
Post a Comment