TAASISI YA INTERPLAST YA NCHINI UHOLANZI YAENDESHA WARSHA KUKABILIANA NA UGONJWA WA FISTULA ZANZIBAR
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Saleh Jidawi Akifungua Warsha ya
kuwajengea uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na Mangariba juu ya
Kutahiri watoto wa kiume ili kuepukana na Ugonjwa wa Fistula.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Interplast ya nchini Uholanzi Dkt. Rein Zeeman kushoto
akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya Waandishi wa habari juu ya mafunzo ya
kuwajengea uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na Mangariba juu ya
Kutahiri watoto wa kiume ili kuepukana na Ugonjwa wa
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Saleh Jidawi katika picha ya
pamoja na Wanachama wa Taasisi ya Interplast baada ya Ufunguzi wa Warsha
ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Wizara ya Afya na Mangariba juu ya
Kutahiri watoto wa kiume ili kuepukana na Ugonjwa wa Fistula.Fistula Zanzibar. PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Interplast ya nchini Uholanzi Dkt. Rein Zeeman
aliyesimama mbele akiendesha Warsha ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa
Wizara ya Afya na Mangariba juu ya Kutahiri watoto wa kiume ili
kuepukana na Ugonjwa wa Fistula.
======== ======== =====
Faki Mjaka- Maelezo Zanzibar .
Taaluma
ndogo katika kutahiri Watoto wa kiume imeelezwa kuwa ni miongoni mwa
Vyanzo vya Ugonjwa wa Fistula ambapo Watoto waliotahiriwa huwa na njia
zaidi ya moja ya kupitishia Mkojo.
Hali
hiyo imepelekea Taasisi ya Interplast ya nchini Uholanzi kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya kuandaa Warsha ili kukabiliana na tatizo
hilo kwa Watoto wa Zanzibar.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Warsha hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.
Mohammed Saleh Jidawi amesema ni vyema Mangariba wakapatiwa mafunzo
kutoka kwa Wataalam ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Amesema
kupatikana kwa taaluma ya kutosha kutalifanya tatizo hilo kupungua na
kupelekea Afya za watoto kuimarika.
“Sisi
Serikali kazi yetu ni kuhakikisha Wananchi wanaondokana na Matatizo
ndio maana tukashirikiana na Taasisi hii ya Interplast ili kuwajengea
uwezo Mangariba wetu juu ya tatizo la Fistula” alisema Dkt. Jidawi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Interplast Dkt. Rein Zeeman amesema
wamekuja Zanzibar kwa ajili ya kutoa elimu na ushauri ili Mangariba
waweze kupata mbinu bora za kufanya kazi zao. Amefahamisha kuwa Jamii
inapaswa kuelewa kwamba kazi ya Kutahiri inahitaji kufanywa kwa taaluma
na tahadhari kubwa kama inayochukuliwa katika Upasuaji wa binadamu.
“Jamii
inapaswa kujua kuwa Kutahiri ni jambo la hatari na hivyo linapaswa
kufanywa tu na watu waliopatiwa mafunzo ya kutosha” Alisisitiza Dkt.
Zeeman. Naye Mshauri wa Taasisi ya Interplast Bi. Ruth Lester amesifia
mashirikiano ya kutosha wanayoyapata kutoka kwa Wananchi na Serikali kwa
ujumla.
Ameongeza
kuwa matarajio yao nikuona kazi ya Ungariba haifanywi na kila mtu
badala yake ifanywe na Wataalam waliosajiliwa ili kuepukana na Tatizo la
Fistula kwa Watoto. Amesema utafiti waliofanya wamegundua kuwa kila
Watoto 1,000 Wakiume waliotahiriwa Zanzibar wawili hadi watatu wamepata
tatizo la Vistula kutokana na kutahiriwa vibaya.
“Tumefanya
utafiti katika sehemu mbali mbali duniani kuhusu kutahiri,kwa mfano Mji
wa Birmingham Watoto 50,000 waliotahiriwa hakuna aliyegundulika na
tatizo lakini kwa Zanzibar kila Watoto 1,000 Wawili hadi watatu wamepata
tatizo” Aliongeza Dkt. Semina hiyo ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa
Afya na Mangariba imefanyika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View mjini Unguja
ambapo pia itaendelea katika Kisiwa cha Pemba ili kuondokana na ugonjwa
wa Fistula kwa Watoto Zanzibar. IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
TAASISI YA INTERPLAST YA NCHINI UHOLANZI YAENDESHA WARSHA KUKABILIANA NA UGONJWA WA FISTULA ZANZIBAR
Reviewed by crispaseve
on
21:59
Rating:
Post a Comment