Watanzania waaswa kudumisha na kuuenzi muungano.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai .
(Na Jovina Bujulu, MAELEZO DODOMA).
Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar ni jambo la kujivunia kwa watanzania wote na katika bara la Afrika.
Hayo
yamesemwa leo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Job Ndugai wakati
wa mahojiano katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha
Televisheni cha TBC ONE.
Mh.
Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alisema kuwa jambo la Muhimu tunalotakiwa kufanya kwa sasa ni
kuimarisha na kuboresha Muungano ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo.
“Hatuna
budi kuendelea kuuimarisha muungano uliopo ikiwa ni kichocheo cha
maendeleo, tumeona mifano kwenye nchi kadha wa kadha zilizo katika
muungano mfano nchi Marekani imekuwa mfano bora duniani kimaendeleo hasa
kutokana na Muungano uliopo” Alisema Ndugai.
Mh.
Ndugai aliongeza kuwa hata Muasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius
Nyerere alikuwa akitukumbusha mara kwa mara kuusimamia muungano wa
Tanzania na kuudumisha.
“Muasisi
wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiasa Watanzania
wote kuudumisha Muungano wa Tanzania na kuepuka viashiria vyote
vinavyoonekana kuvunja muungano, hivyo tushikamane katika kuudumisha”.
Alisema Ndugai.
Naye
Mjumbe wa Bunge hilo ambaye mjumbe wa secretariati ya marekebisho
kanuni za Bunge Maalum Mhesh. Evod Mmanda alisema kwamba miaka 50 ya
muungano ni faraja na jambo la kujivunia.
“hatuna
budi kwa pamoja kukaa na kuufikiria zaidi Muungano na kutatua
changamoto zote zinazojitokeza ili kuudumisha muungano huu na Wasiopenda
Muungano hawana sababu za kutosha” Alisema Mh. Mmanda.
Watanzania waaswa kudumisha na kuuenzi muungano.
Reviewed by crispaseve
on
22:01
Rating:
Post a Comment