FULL TIME GERMANY 7-1 BRAZIL FIFA 2014

Luiz akilia baada ya kushindwa na Ujerumani
Nahodha
wa muda wa Brazil David Luiz amewataka mashabiki wa tim,u hiyo kote
duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani Selecao ilipoadhibiwa
kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu
fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Amini Usiamini Ujerumani ilikuwa inaongoza mabao 5-0 kufikia dakika 29 ya kipindi cha kwanza .
"Wajerumani walikuwa timu bora zaidi yetu''
Luiz,ambaye
alitajwa kama nahodha wa muda baada ya marufuku ya Nahodha Thiago Silva
kumlazimu kutizama tu mechi hiyo alisema hawjui kilichotendeka lakini
ni wakati wao kujifunza kutokana na aibu hiyo ya kusakamwa 7-1. "Ni siku
ya majonzi tele kwa wabrazil''.

Luiz akilia baada ya kushindwa na Ujerumani
"Mtuwieni radhi sijui tutafanya nini ilituwaone tena wabrazil wakitabasamu,?
Kilio
kimezidi kote nchini humo haswa baada ya nyota wa Brazil Neymar
kujeruhiwa uti wa mgongo Ijumaa iliyopita katika mechi ya kufuzu kwa
nusu fainali dhidi ya Colombia.
Kwa Upande wake Kipa wa Brazil Julio Cesar alitaja dakika hizo kumi timu hiyo ilipofungwa mabao manne kuwa sawa na kuzimia.
''Sio jambo unaloweza kujieleza.

Julio Ceasar; Ujerumani ilikuwa timu bora
Kombe hili la dunia limekuwa lenye ufanisi hadi leo.
Hata hivyo tunawashukuru Wabrazil kwa kutuunga mkono katika kipindi hichi chote .
Hata wachezaji wakiomba msamaha kwa kichapo hichi cha leo ,ni wazi kuwa mjerumani alituzidi maarifa .
Lazima tukali hilo walikuwa bora kutuliko leo.'''
FULL TIME GERMANY 7-1 BRAZIL FIFA 2014
Reviewed by crispaseve
on
15:20
Rating:
Post a Comment