Ugeni wa benki ya maendeleo ya china watembelea ofisi ya rais, tume ya mipango
*Yazungumzia
uwezekano wa kugharamia utekelezaji wa miradi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025
Na Saidi Mkabakuli
Ugeni kutoka Benki
ya Maendeleo ya Uchina umetembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa minajili
ya kuja kujadiliana juu ya uwezekano wa kugharamia miradi ya maendeleo kwa
upande wa barabara, kilimo na nishati ili kuiwezesha Tanzania kufikia lengo
lake la kuwa nchi ya uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.
Ugeni huo unaongozwa
na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Jiang Zhigang utatembelea wizara mama
zinazosimamia miradi itakayogharamiwa na Benki hiyo ambazo ni pamoja na Wizara
ya Kilimo, Wizara ya Uchukuzi na Wizara Nishati na Madini.
“Tumekuja Tanzania
kwa ajili ya kukagua na kujionea maendeleo ya sekta za kipaumbele ambazo
tutagharamia ili kupata uelewa wa gharama halisi ya miradi hiyo,” alisema Bw. Zhigang.
Kwa mujibu wa
makubaliano ya awali yaliyofanyika mwezi Julai, 2012 kati ya taasisi hizi
mbili, Tume ya Mipango imekubali kupatiwa utaalamu elekezi kwenye maeneo hayo
wenye lengo la kukuza ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizo.
Wakati huo huo,
imebainika kuwa Tanzania imekuwa kinara katika kuvutia uwekezaji wa ndani na
nje ya nchi miongoni mwa nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara kutoka asilimia
18 ya Pato la Taifa (GDP) kwa mwaka 2002 hadi kufikia asilimia 34 kwa mwaka
2013.
Hayo yamewekwa wazi
na Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (anayeshughulikia
Biashara za Kimataifa na Mashirikiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe wakati
akiwasilisha mada ya Hali ya Uchumi wa Tanzania wakati Ugeni kutoka Benki ya
Maendeleo ya Uchina ulipoitembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
“Tunajitahidi
kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi, kwa mfano, mwaka 2003 tuliweza
kuvutia uwekezaji kutoka nje ‘Foreign Direct Investment (FDI)’ wa jumla ya Shilingi za Kimarekani milioni 308.2,
na mwa 2013 zilifikia Shilingi za Kimarekani milioni 1,872.4,” aliongeza.
CAPTIONS
Mwenyekiti wa Majadiliano
kati ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Benki ya Maendeleo ya Uchina,
Bw. Maduka Paul Kessy (Wapili Kulia) akizungumza wakati wa Majadiliano. Kulia ni
Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (anayeshughulikia
Biashara za Kimataifa na Mashirikiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe. Wengine
pichani ni wajumbe wa majadiliano, Bi. Martha Luanda (Kushoto) kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Bw. Medard Ngaiza (Wapili Kushoto), kutoka
Dawati la Uchina, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu wa
Benki ya Uchina, Bw. Jiang Zhigang (Katikati) akisisitiza jambo wakati
walipokuwa na mazungumzo na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Kushoto
ni Mtafiti Kutoka ‘State Information Center’, Bw. Chen Qiang na Kulia ni Bw. Zhao
Bingjie, Mhandisi Mwandamizi kutoka ‘Railway Third Survey and Design Institute
Group’.
DSC06455
Mkurugenzi Mkuu wa
Benki ya Uchina, Bw. Jiang Zhigang (Katikati) akiongoza mjadala wakati wa
majadiliano na na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (Hawapo pichani)
juu ya uwezekano wa Benki hiyo kufadhili baadhi miradi ya maendeleo nchini.
Naibu Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (anayeshughulikia Biashara za
Kimataifa na Mashirikiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe (Kulia) akibadilisha mawazo
na Ugeni
kutoka Benki ya Maendeleo ya Uchina
(Hawapo pichani) wakati walipotembelea Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango .
Naibu Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (anayeshughulikia Biashara za
Kimataifa na Mashirikiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe (Kushoto) akiwasilisha Mada ya Hali ya
Uchumi wa Tanzania wakati Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Uchina ulipoitembelea
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Wakili wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Wakili Nyanzala Nkinga (Katikati) akifafanua jambo kwa
mmoja kati ya wajumbe wa majadiliano, Bibi Martha
Luanda (Kulia). Kushoto ni Bi. Gloria
Ngowi.
Picha
na Saidi Mkabakuli
Ugeni wa benki ya maendeleo ya china watembelea ofisi ya rais, tume ya mipango
Reviewed by crispaseve
on
03:09
Rating:
Post a Comment