Header AD

WATU 16 WAFA AJALI WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA


Baadhi ya miili ya marehemu.
Watu  zaidi ya 17 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa  baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka k ijiji  cha Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea leo hii jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda  Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri  T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani   Sikonge.Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo a kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi( Day-worker)
Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la  Sabena lililokuokea  Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea  Mwanza kwenda Mpanda.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.
WATU 16 WAFA AJALI WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA WATU 16 WAFA AJALI WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA Reviewed by crispaseve on 06:20 Rating: 5

No comments

Post AD