MEMBE MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA
Mwenyekiti
wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari jijini Dar es salaam jana (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya
tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Jimmy Charles. (Picha na Francis Dande)
Msama akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Jimmy Charles akifafanua jambo.
………………………………………………………………………………..
WAZIRI wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka
huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa kamati
ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya tamasha
hilo yamekamilika kwa asilimia 97 hivyo amewataka wananchi kujitokeza
kwa wingi siku hiyo.
Alisema wameshakamilisha maandalizi ya tamasha hilo, ila kinachosubiriwa ni waimbaji wa kimataifa Ephraim Sekeleti wa Zambia, Ifeanyi Kelechi kutoka Uingereza, Rebeca Malope na Thori Mahlangu wote kutoka Afrika Kusini pamoja na Faustine Munishi ‘Malebo’ kuanza kuwasili
nchini.
nchini.
“Tamasha la
mwaka huu litakuwa la aina yake kwani tutakata keki, kupiga fataki kama
ishara ya kutakiana amani, upendo na mshikamano na tutaiombea nchi
yetu kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu’’alisema
Msama.
Msama aliongeza kuwa tamasha la mwaka huu litabeba ujumbe mahsusi wa ‘amani na upendo ndio amani kwa watanzania’, aidha tamasha hilo pia litatumika kupiga vita maauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’.Aliongeza kuwa ukiachia mgeni Waziri Membe, pia wageni mashuhuri watahudhuria tamasho hilo akiwemo rais mstaafu ali Hassani Mwinyi ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa.
MEMBE MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA
Reviewed by crispaseve
on
04:00
Rating:
Post a Comment