IMETOSHA yaendeleza mkakati wake kimataifa kusafisha jina la nchi
Mkakati
wa kutokomeza unyanyapaa na mauaji ya watu wenye ualbino nchini, uitwao
IMETOSHA, jana ulianza rasmi kujitokeza kimataifa baada ya kushiriki
katika pambano la kimataifa la kirafiki kati ya nyota wa zamani wa
Barcelona na Veterani wa Afrika Mashariki.
Katika
mpambano huo wa kimataifa uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mkangara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck
Sadick na maafisa kutoka katika mkakati huo walipata nafasi ya kuongea
na wachezaji hao nyota wa Barcelona kuhusiana na dhana iliyoko katika
nchi za nje ambako inaaminika Tanzania wanauana wenyewe kwa wenyewe
kutokana na imani za kishirikina.
Akiongea
baada ya mpambano huo ambapo Barcelona waliibuka washindi, Balozi na
muasisi wa mkakati huo unaoelekea na sura ya kizalendo na kitaifa, Bw.
Henry Mdimu alisema kulikuwa na haja wachezaji hawa warudi na ujumbe
kwao wenye majibu ya maswali wanayojiuliza kuhusiana na mauaji ya albino
na kukosa majibu.
"Maneno
haya ya kwamba sisi tunauana kwa imani za kishirikina, ingawa matukio
mengi yapo kanda ya Ziwa lakini nchi nzima inachafuka kwa hiyo haja ya
kusafisha jina la nchi kwa mataifa ya nje ipo na sisi IMETOSHA tumeamua
kuchukua jukumu", alisema Balozi huyo ambaye pia ana ualbino.
Mdimu alibainisha kwamba katika mkakati wa kimataifa wameanza kwa kuanzisha tovuti (imetosha.or.tz)
ambayo itakuwa ikionesha matukio mbali mbali yanayopinga mauaji na
unyanyapaa ili wanaoamini vingine waone kwamba unyanyapaa na mauaji kwa
watu wenye ualbino si kitu ambacho watanzania kama taifa wanakifurahia.
Balozi
huyo pia alitoa wito kwa kila mtanzania kuuunga mkono mkakati wa
IMETOSHA ili katika miaka 20 ijayo kizazi kijacho kiwe na jamii yenye
watu wenye ualbino wanaoishi kwa amani katika nchi yao.
Wachezaji
wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania wakiongozwa na Patrick
Kluivert (aliebeba mtoto) wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu
ya Tanzania Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja
wa Taifa, Jijini Dar es salaam. hadi mwisho wa mchezo, Barcelona ya
Hispania ilishinda bao 2-1.
Mchezaji
wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert akifurahia
jambo na Mtoto Sharifa mwenye Ualbino kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa
kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa,
Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara (wa pili
kulia) akizungumza jambo na Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya
Hispania, Patrick Kluivert wakati akiwasalimia wachezaji hao kabla ya
kuanza kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans, uliopigwa
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana.Kulia ni Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam, Said Meck Sadick.
Sehemu
ya Wachezaji wa timu ya Tanzania Veterans na Barcelona wakiwa kwenye
picha ya pamoja na Watoto wenye Ualbino mbele ya Bango la Mkakati wa
kutokomeza unyanyapaa na mauaji ya watu wenye ualbino nchini, uitwao
IMETOSHA.Habari/Picha na Othman Michuzi
IMETOSHA yaendeleza mkakati wake kimataifa kusafisha jina la nchi
Reviewed by crispaseve
on
05:47
Rating:
Post a Comment