Header AD

MSD YABORESHA HUDUMA ZA UTOAJI TAARIFA KWA WATEJA WAKE.

Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda Bohari ya dawa (MSD), Edward Terry,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa habari MAELEZO jijjini Dar es Salaam leo kuhusu utendaji na mipango ya Bohari ya Dawa (MSD) na Ofisa Uhusiano Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),Etty Kusiluka.

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
 BOHARI ya dawa (MSD) imeboresha huduma  kwa wateja wake kwa kutoa taarifa zinazomhusu mteja kwa kuziweka wazi katika tovuti yao.
 Akizungumza na wandishi wa habari  katika ukumbi wa  Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry,  amesema kuwa taarifa hizo ni za mali inayopatikana gharani, taarifa za kiasi cha fedha za wateja kilichopo katika kila akaunti,fomu za marejesho pamoja na bei za bidhaa na bei zake.

Pia Terry amesema kuwa wateja wenye mahitaji ya dawa au vifaa wanatakiwa kuandika barua kuelezea mahitaji yao pamoja na maelekezo mhimu ya kifaa husika na kutatuliwa na kitengo cha manunuzi ya bohari hiyo.
MSD YABORESHA HUDUMA ZA UTOAJI TAARIFA KWA WATEJA WAKE. MSD YABORESHA HUDUMA ZA UTOAJI TAARIFA KWA WATEJA WAKE. Reviewed by crispaseve on 06:48 Rating: 5

No comments

Post AD