TIMU YA HARAKATI YA IMETOSHA YATEMBELEA KITUO CHA BUHANGIJA, MKOANI SHINYANGA
Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga.
Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha
ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za
Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji
kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.
Akiongea
na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za Imetosha Masoud Ali
(Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa kila
binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na
unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. “Tunatambua hapa kati yenu
kuna vipaji vya aina mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati
za kupinga na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa
kuwatia moyo kuwa mna uwezo mkubwa ndani yenu hivyo
msijidharau” alisema Masoud.
Wajumbe wa Imetosha
BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI |
TIMU YA HARAKATI YA IMETOSHA YATEMBELEA KITUO CHA BUHANGIJA, MKOANI SHINYANGA
Reviewed by crispaseve
on
06:28
Rating:
Post a Comment