UMOJA WA TAASISI ZA HIJJA ZANZIBAR ZAANDAA KONGAMANO KWA MAHUJAJI WATARAJIWA
Mwenyekiti
wa Bodi ya Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar Sheikh Abdulhamid
akifungua Kongamano la mahujaji watarajiwa katika ukumbi wa Beit al
Yamin Malindi Zanzibar, kulia yake ni Mwenyekiti wa Umoja huo na kushoto
Sheikh Othman Maalim.Katibu wa UTAHIZA Ustaadh Ali Adam akitoa historia ya Umoja huo na kazi zake katika kongamano lililofanyika Malindi ZanzibarBaadhi
ya mahujaji watarajiwa wakimsikiliza Sheikh Othman Maalim
alipowasilisha mada ya umuhimu wa kutekeleza ibada ya hija na madhara ya
kuchelewesha kutekeleza ibada hiyo katika kongamano liliofanyika
Malindi Mjini Zanzibar.
………………………………………………………………………………….
Na Ramadhani Ali –Maelezo Zanzibar
Waislamu
wa Zanzibar wanaotegemea kutekeleza Ibada ya Hijja mwaka huu
wameshaurfiwa kukamilisha mipango ya safari hiyo mapema ili kuziwezesha
Taasisi zinazosafirisha mahujaji kuweza kukamilisha taratibu mpya
zilizowekwa na Serikali ya Saudi Arabia.
Akizungumza
katika Kongamano la mahujaji watarajiwa lililofanyika ukumbi wa Beit
al Yamin Malindi, Afisa kutoaka Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana
Ustaadh Khalid Mohammed Mrisho amesema Serikali ya Saudi Arabia imefanya
mabadiliko makubwa ya taratibu za maandalizi ya Hijjah kuanzia mwaka
huu.
Amesema
wamefanya maamuzi hayo baada ya malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na
mahujaji kutokana na vitendo vya udanganyifu vilivyokuwa vikifanywa na
baadhi ya Taasisi zinazosafirisha mahujaji kutoka mataifa mbali mbali
duniani.
“Baadhi
ya viongozi wa Taasisi zinazosafirisha mahujaji walikuwa wakiwatoza
fedha mahujaji wao kwa ajili ya kulipia Viwanja vya ndege vya Makka na
Madina lakini walikuwa hawalipi na mahujaji kuzuiliwa kwa saa
kadhaa,”alisema Ustaadh Khalid.
Taasisi
nyengine alisema zilikuwa zinawaahidi mahujaji kuwakodia nyumba nzuri
za karibu katika miji mitakatifu ya Makka na Madina lakini wanapofika
huko huwekwa kwenye nyumba mbovu na wengine hukosa huduma ya chakula.
Amesema
katika kukabiliana na matatizo hayo Serikali ya Saudia Arabia kuanzia
sasa imeziagiza Taasisi zinazosafirisha mahujaji kufanya taratibu zote
za maandalizi ya safari, makaazi na matembezi kwa njia ya mtandao na
kulipa gharama zote wakiwa nchini mwao.
Amesema
iwapo taratibu hizo hazikukamilika hujaji atakosa visa ya kuingia Saudi
Arabia na atakuwa amekosa kutekeleza ibada ya Hijjah kwa mwaka huo.
Ameongeza
kuwa mwaka huu nchi hiyo imeweka hadi tarehe 27 Juni kuwa ni siku ya
mwisho kukamilisha taratibu za mahujaji na baada ya tarehe hiyo mtandao
huo utakuwa umefungwa na itakuwa hakuna njia nyengine.
“Lengo
la uwamuzi huo wa Saudi Arabia ni kuwaondoshea mahujaji usumbufu
usiowalazima wakati wa kutekeleza ibada hiyo,”alisisitiza Ustaadh
Khalid.
Amewakumbusha
mahujaji watarajiwa kuwa waangalifu na mizigo yao wakati wa safari na
wanapokuwa nchini humo na watakaporejea kuchukua kiwango cha mizigo
kinachokubalika kwenye ndege.
Akifungua
Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar
(UTAHIZA) Mwenyekiti wa Bodi Sheikh Khamis Abdulhamid amewasisitiza
waislamu wenye uweze kutekeleza ibada ya hijja ili kukamilisha uislamua
wao.
Mwaka
huu Tanzania imepewa nafasi 3,000 kupeleka mahujaji nchini Saudi
Arabia ambapo ibada hiyo hutekelezwa kila mwaka mwezi wa mfunguo tatu
UMOJA WA TAASISI ZA HIJJA ZANZIBAR ZAANDAA KONGAMANO KWA MAHUJAJI WATARAJIWA
Reviewed by crispaseve
on
00:37
Rating:
Post a Comment