Watatu wajishindia mamilioni kutoka Bayport
Meneja Utawala wa Bayport Financial Services aliyezibwa macho, Evalyine
Hall, akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa Kopa Bayport kwa njia ya
mtandao wa www.kopabayport.co.tz,
inayoendeshwa na taasisi hiyo ambapo washindi watatu ambao ni Hyasint
Mbunda (Songea), Phaustine Mbilinyi (Dar es Salaam) na Allen Bishubo
(Bukoba), walipatikana na kila mmoja kushinda Sh Milioni moja. Kushoto
ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo na kushoto ni
Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein. Picha na Mpiga
Picha Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WASHINDI watatu waliokopa fedha kwa njia ya Mtandao wa Taasisi ya Kifedha ya
Bayport Financial Services, wamejishindia Sh Milioni moja kila mmoja, kutokana
na shindano hilo lililoanzishwa maalum kwa ajili ya wateja wao waliomua
kuutumia mtandao wao wa www.kopabayport.co.tz kupata huduma mbalimbali.
Washindi hao wamepatikana kutoka kwenye droo ya mwezi wa Aprili, iliyoendeshwa
na Bayport Financial Services kwa kusimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania.
Meneja
Utawala wa Bayport Financial Services Evelyine Hall katikati akisoma
koponi ya mmoja wa washindi wa Kopa Bayport kwa njia ya Mtandao
inayoondeshwa na taasisi hiyo ya kifedha. Kulia kwake ni Msimamizi wa
Michezo ya Kubatisha Tanzania, Humud Abdulhussein na kushoto ni Ngula
Cheyo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi hiyo ya Bayport Financial
Services.
Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial
Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba washindi hao watatu wamepatikana baada ya
kuamua kukopa kwa njia ya mtandao wao waliyouzindua mwezi uliopita.
Ngula
Cheyo (katikati) ambaye ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa taasisi ya
kifedha ya Bayport Financial Services akizungumza jambo katika droo ya
kutafutwa washindi watatu wa bahati nasibu inayoandaliwa na taasisi hiyo
ambao kila mmoja alishinda Sh Milioni moja.
“Tuliamua kuanzisha huduma ya kukopa kwa njia ya mitandao tukiamini ni huduma
rahisi inayoweza kuwafanya Watanzania wote wafurahie kwa pamoja na kukuza
uchumi wetu, hivyo tukaona tufike mbali zaidi kwa kuchezesha droo yetu ya
kuwapatia Sh Milioni moja washindi watatu kila mwezi.
Ngula
Cheyo (katikati) ambaye ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa
taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services akizungumza jambo
katika droo ya kutafutwa washindi watatu wa bahati nasibu inayoandaliwa
na taasisi hiyo ambao kila mmoja alishinda Sh Milioni moja. Kulia ni
Humud Abdulhussein kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha na kushoto ni
Meneja Utawala wa Bayport Financial Services, Evalyine Hall.
Shughuli ya kutafutwa washindi wa Kopa na Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz inaendelea.
Jamani
huyu ndiye mshindi. Ndivyo anavyoenekana kusema Meneja Utawala wa
Bayport Financial Services katika droo ya kutafutwa washindi watatu
waliokopa kwa njia ya mtandao.
Washindi hao ni Phaustine Mbilinyi (Dar es Salaam), Hyasint Mbunda (Songea) na
Allen Bishubo (Bukoba)ambao kila mmoja amejinyakulia Sh Milioni moja baada ya
kushinda katika bahati nasibu yetu hii, huku tukiamini kuwa wateja wengine
wanao uwezo wa kushinda katika droo nyingine ijayo, ukizingatia kuwa Bayport
ipo kwa ajili yao katika kutoa huduma bora zinazoweza kuwakwamua, ikiwamo ya
mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana,” alisema Cheyo.
Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka kwenye Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein alisema washindi hao baada ya
kupatikana walipigiwa simu ili wataarifiwe ushindi wao na jinsi ya kupata
zawadi zao za Sh Milioni moja kila mmoja.
“Huduma ya kukopa kwa njia ya mtandao inayoendeshwa na Bayport Financial
Services ni nzuri na rahisi, ambapo pia ipo fursa ya kushinda pesa taslimu kwa
wale watakaoamua kukopa kwa njia hiyo,” alisema.
Bayport Financial Services ni taasisi ya kifedha inayoongoza kutoa mikopo
isiyokuwa na dhamana wala amana kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni
zilizoidhinishwa na taasisi hiyo.
Watatu wajishindia mamilioni kutoka Bayport
Reviewed by crispaseve
on
10:20
Rating:
Post a Comment