Waziri Mkuu mstaafu John Malecela, amesema kushabikia wanasiasa wanaojipitisha na kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kabla ya wakati, ni sawa na kupoteza muda, kwani nchi bado in mambo mengi ya maendeleo yanayopaswa kufanywa, kabla ya uchaguzi mkuu.
Malecela ambaye amewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa
Rais na ni kada wa CCM, alisema hayo jana alipotakiwa kutoa maoni yake
kuhusu makada wa chama hicho wanaojipitisha kwa makundi mbalimbali
wakitaka waungwe mkono.
“Wananchi wengi wangependa kupata habari za
maendeleo kwa ujumla na ni vyema tukaiga mfano wa Uingereza ambako
pamoja na kwamba wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu, watu bado
wanazungumzia mambo mengine ya maendeleo,” alisema Malecela.
Alihoji,”hapa kwetu ni tofauti, kila siku watu
wanazungumzia uchaguzi, kwanini tusiendelee kuzungumzia maendeleo
kwanza, halafu masuala haya ya uchaguzi yasubiri muda wake?”
Malecela alisema uchaguzi mkuu hausitishi shughuli
zingine za maendeleo, hivyo jamii inapaswa kuendelea kuwajibika katika
shughuli hizo badala ya kuweka akili na mawazo yao yote kwenye uchaguzi
mkuu ambao hata muda haujafika.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
nyumbani kwake mjini Dodoma mapema mwaka jana Malecela alisema
Sekretarieti ya CCM inapaswa kuwachukulia hatua kali makada
wanaojipitisha maeneo mbalimbali nchini kwa nia ya kusaka urais, kabla
ya chama hicho kupanga muda.
Malecela ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Ushauri
la Taifa la CCM, aliwafananisha walioanza mbio za urais kupitia CCM na
watu wanaowahi kukimbia kabla ya kipenga kupigwa na kusema hawawezi
kupimwa sawa na wale wanaosubiri kuanza rasmi kwa kampeni.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea...
Waziri Mkuu mstaafu John Malecela, amesema kushabikia wanasiasa wanaojipitisha na kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kabla ya wakati, ni sawa na kupoteza muda, kwani nchi bado in mambo mengi ya maendeleo yanayopaswa kufanywa, kabla ya uchaguzi mkuu.
Reviewed by crispaseve
on
03:21
Rating:
Post a Comment