ActionAid yakutanisha wadau kujadili malengo mapya ya milenia
Wakili
wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus Michael
Kulaya akiwasilisha mada katika semina iliyoandaliwa na taasisi ya
Landesa.
Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus
Michael Kulaya (mbele) akiwasilisha mada katika semina iliyoandaliwa na
taasisi ya Landesa.
Mwakilishi wa taasisi ya Landesa na ActionAid akizungumza kufungua
semina ya wadau mbalimbali kutoka asasi na mashirika ya kutetea jamii
kwa ajili ya kujadili malengo mapya ya milenia 'Post 2015 Sustainable
Development Agenda.
Baazi ya washiriki wa semina hiyo kutoka asasi na mashirika ya kutetea
jamii kwa ajili ya kujadili malengo mapya ya milenia 'Post 2015
wakifuatilia mada anuai.
Baazi ya washiriki wa semina hiyo kutoka asasi na mashirika ya kutetea
jamii kwa ajili ya kujadili malengo mapya ya milenia 'Post 2015
wakifuatilia mada anuai.
Baazi ya washiriki wa semina hiyo kutoka asasi na mashirika ya kutetea
jamii kwa ajili ya kujadili malengo mapya ya milenia 'Post 2015
wakifuatilia mada anuai.
Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus
Michael Kulaya akijibu maswali ya washiriki semina hiyo. Kulia ni Ofisa
Uchumi, Andrew Aloyce kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Mwakilishi kutoka UN Women, Bi. Usu Mallya akiwasilisha mada yake katika semina hiyo kwa washiriki.
ACTIONAid
kwa kushirikiana na taasisi ya Landesa imekutanisha wadau mbalimbali
kutoka asasi na mashirika ya kutetea jamii kwa ajili ya kujadili malengo
mapya ya milenia 'Post 2015 Sustainable Development Agenda'
yanayotarajiwa kutekelezwa kwa nchi zilizokubaliana.
Akiwasilisha mada Ofisa Uchumi, Andrew Aloyce kutoka Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango alisema serikali imejipanga vema katika kutekeleza malengo
mapya 17 ya Milenia yaliyopendekezwa ikiwa ni pamoja na kushirikisha
asasi za kijamii na wananchi katika kuyatekeleza kila mmoja na nafasi
yake.
Alisema
licha ya malengo ya sasa ya milenia kuwa mengi tofauti na yaliyopita
lakini utekelezaji wake kwa kila moja unategemeana huku yakiwa
yamechambuliwa zaidi pamoja na kuingizwa kwenye mipango ya maendeleo
katika utekelezaji wake jambo ambalo litachangia mafanikio kwenye
utekelezaji wa kila lengo.
"...Malengo mapya ni mengi lakini ukisoma kwa undani kila lengo
linaingiliana na lingine, hakuna linalosimama peke yake...na pia ya sasa
yamechambuliwa zaidi," alifafanua Aloyce akifafanua zaidi baada ya
wanasemina kuonesha hofu ya utekelezwaji wa malengo mapya kutokana na
wingi wake.
Alisema
Serikali inaendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kushiriki
kiufasaha katika utekelezaji wake, kwani kila mwananchi wakiwemo
wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara kila mmoja ananafasi yake
katika kufanikisha malengo hayo.
Aidha aliongeza licha ya kutofanikiwa vizuri kwa malengo yaliyopita
lakini yapo baadhi ya maeneo nchi ilifanya vizuri sana hasa kwenye elimu
na kupunguza umasikini kwa jamii.
Alisema
maeneo ambayo yalikuwa na changamoto kubwa ni katika malengo yaliyogusa
upunguzaji vifo vya akinamama wajawazito pamoja na vifo vya watoto
chini ya miaka mitano.
Kwa upande wake, Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Honestus Michael Kulaya akiwasilisha mada juu ya haki za
wanawake katika suala zima la umiliki wa ardhi nchini alisema migogoro
mingi ya ardhi bado inachangiwa na jamii kutokuwa na utamaduni wa
kuandika usia kabla ya kifo.
Alisema
suala la kujenga utamaduni wa kuandika usia ni jambo la msingi ambalo
linapaswa kuzingatiwa ili kupunguza migogoro ndani ya familia, kwani
kufanya hivyo mapema hakuna uhusiano na kukaribia kufa. Alibainisha kuwa
watu wengi hawapendi kuandika usia mapema na wengine hudhani kuandika
usia basi umekaribia kufa jambo ambalo si kweli.
Alisema kwa sasa Serikali imejitahidi kujenga usawa kati ya wanawake na
wanaume katika umiliki ardhi lakini changamoto iliyopo bado akinamama
wengi wanaofanikiwa kupewa ardhi wamekuwa hawaiendelezi na kungoja
kuiuza hapo baadaye.
Alisema
taratibu zote zipo wazi na pale inapotakiwa kundi hilo kupewa ardhi
hupata bila vikwazo vyovyote tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.
Awali mwakilishi wa taasisi ya Landesa linalofanya kazi kwa ushirikiano
na ActionAid alisema shirika hilo limekuwa likiwajengea uwezo jamii hasa
makundi ya wanawake ili kuweza kupigania haki anuai za msingi kwao
pamoja na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali dhidi yao. Pamoja na
kusaidi kampeni za usawa wa umiliki ardhi katika maeneo mbalimbali.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
ActionAid yakutanisha wadau kujadili malengo mapya ya milenia
Reviewed by crispaseve
on
04:32
Rating:
Post a Comment