ATCL yarejesha safari zake kuelekea Mwanza.
Abiria
wakipanda kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina
ya CRJ-200 tayari kuelekea Mwanza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha
safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo
tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo
litafanya safari zake kati ya majiji hayo mawili mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.
Abiria
wakishuka toka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL)
aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege wa Mwanza Jumamosi jioni baada ya
shirika hilo kurejesha safari zake kuelekea jijini Mwanza baada ya kusimamisha
safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika
hilo litafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza mara mbili kwa siku katika siku zote saba za
wiki.
Abiria
wakipanda kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina
ya CRJ-200 tayari kuelekea jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Mwanza
Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kati ya Dar es
Salaam na Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka
jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati majiji
haya mawili mara mbili kwa siku
katika siku zote saba za wiki.
SHIRIKA la ndege la taifa (ATCL) limerejesha
safari zake kuelekea mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kupanua
huduma kwa wateja wake hapa nchini.
Safari ya kwanza ya shirika hilo
kuelekea mkoani Mwanza ilifanyika mwishoni mwa juma lilopita kwa kukutumia
ndege yake aina ya CRJ- 200, baada ya safari hizo kusimama tangu mwezi Agosti
mwaka mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari mara
tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza, Kaimu Afisa
Uhusiano wa Shirika hilo, Bi Lily Fungamtama alisema uamuzi wa kurejesha safari
hizo umezingatia mahitaji ya wateja wa shirika hilo.
“Tumepokea maombi mengi kutoka kwa wateja wetu wakiwemo
wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwa kuhusisha majiji haya mawili. Kwa
kuwa ATCL ni shirika mama la ndege hapa nchini tukafanya kila jitihada
kuhakikisha tunarejesha safari zetu kuelekea jijini Mwanza,’’ alibainisha
Fungamtama huku akiongeza kuwa shirika hilo litafanya safari zake mara mbili kwa siku katika siku zote saba za
wiki.
Alisema ili kukabiliana na ushindani wa
kibiashara dhidi ya mashirika mengine ya ndege yanayofanya safari zake kuelekea
mkoani humo, shirika hilo limewekeza zaidi kwenye ubora wa huduma zake sambamba
na kutoa huduma zake kwa gharama nafuu.
Akizungumzia na waandishi wa habari
mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza mmoja wa
abiria waliosafiri na ndege hiyo Bw. Bakari Hamidu mbali na kushukuru kurejeshwa
kwa huduma hiyo pia alionyesha kuridhishwa kwake na ubora wa huduma unaotolewa
na wahudumu wa shirika hilo.
“Nimefurahishwa sana na kurejeshwa wa
huduma hii na zaidi nimefurahishwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa abiria na
wafanyakazi wa shirika hili. Kwa hilo lazima niwapongeze,’’ alisema Bw. Hamidu.
Pamoja na kurejesha
safari hizo za mkoani Mwanza, shirika hilo pia kwa sasa linatoa huduma zake
kuelekea mikoa ya Kigoma, Mtwara na visiwa vya Comoro kwa kutumia ndege yake
aina ya CRJ-100.
“Tunatarajia mambo
yatakuwa mazuri zaidi baada ya kukamilika kwa ukarabati wa ndege yetu nyingine
aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 inayoendelea na ukarabati mkubwa kwenye
karakana iliyopo kwenye uwanja wa Kimataaifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini
Dar es Salaam,’’ aliongeza Fungamtama.
ATCL yarejesha safari zake kuelekea Mwanza.
Reviewed by crispaseve
on
08:43
Rating:
Post a Comment