SERIKALI YASEMA HAKUNA DENI HALALI LA WALIMU AMBALO HALIJALIPWA.
Na Magreth Kinabo- maelezo
SERIKALI
imesema kwamba imeshalipa madeni ya walimu ya kiasi cha Sh. bilioni
5.7 ambayo yaligungulika kihalali kati ya Sh. bilioni 19.6 zilizokuwa
zinadaiwa kudaiwa,hivyo kwa sasa hakuna malalamiko mwalimu ambaye
hajalipwa.
Aidha
Serikali imependekeza kwamba halimashauri zilizowasilisha madeni
ambayo si halali, yenye shaka, au watumishi wasio na madai, madai ya
watumishi wasio na madai, madai ya watumishi waliokwishalipwa na
waliowasilisha madai ya mishahara kama madai yasiyo ya mishahara
wawajibishwe.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Likwelile alisema
hayo wakati akitoa taarifa ya uhakiki wa madeni ya walimu wa shule
za msingi, sekondari na Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Stadi.
Alisema
awali wizara yake ilipokea madai ya walimu kutoka Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(TAMISEMI) na watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Stadi(WEMU)yenye jumla ya Sh. bilioni 19.6 ikiwa Sh. bilioni
17.4 kutoka TAMISEMI na Sh. bilioni 2.1 kutoka WEMU.
“Madeni ambayo hajalipwa ni kwa sababu hakuna kielelezo juu ya madai hayo,” alisema Dkt. Likwelile .
Aliongeza
kwamba wizara yake kupitia Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali,
ilifanya uchambuzi wa awali kwa lengo la kujiridhisha na takwimu
zilizowasilishwa na TAMISEMI kwa kila halimashauri na kwa watumishi wa
WEMU, ambao umeonesha kuwa na shaka na baadhi ya madai.
“Baada
ya uchambuzi wa awali idara iliandaa hadidu za rejea kwa lengo la
kufanya uhakiki wa madai yaliyowasilishwa. Uhakiki huo ulifanywa na
wakaguzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na timu ya wakaguzi wa ndani
chini ya usimamizi wa idara hiyo.
“Matokeo
ya uchambuzi wa awali yalipelekea madai ya walimu na watumishi yasiyo
ya mishahara kupungua kutoka Sh. 19.6 hadi kufikia Sh. bilioni 16.2.,”
alisema.
Alifafanua
kwamba madai hayo yaliyohakikiwa yalihusisha walimu 16,315 kutoka
halimashauri 147 na watumishi, 1,152 kutoka WEMU. Madai yasiyohakikiwa
ni Sh. bilioni 3.3 yakihusisha walimu 1,448 ambao hawakuwa na cheki
namba na walimu 1,834 ambao cheki namba hazikuonekana kwenye orodha ya
malipo ya mishahara ya utumishi wa Serikali.
Dkt.Likwelile
alisema kazi ya uhakiki katika halimashauri na WEMU ilifanyika kuanzia
Machi 12, mwaka huu hadi Aprili 11, mwaka huu.
Aliongeza kwamba matokeo ya uhakiki yameonesha kiasi cha Sh. 5.7 kimekubaliwa na kiasi kilichokataliwa ni Sh.bilioni 10.5.
“Zoezi
hili la uhakiki wa madai limeiwezeshha Serikali kuokoa kiasi kikubwa
cha fedha tofauti na iwapo malipo yangefanyika bila kufanya uhakiki,”
alisisitiza.
Alizitaja baadhi
ya changamoto zilizojitokeza ni kuendelea kuwepo kwa madi ya muda mrefu
kwenye halimashauri , baadhi ya madai kuwasilishwa kama madai ya
mshahara, kutokuwepo kwa kumbukumbu za madai kwenye majalada ya
watumishi, majalada ya walimu kutopatikana na hivyo baadhi ya madai
kutohakikiwa.
Changamoto
nyingine ni baadhi ya madai yaliyokwisha kulipwa kuwasilishwa kama
madai mapya na baadhi ya madai kuwasilishwa zaidi ya mara moja kwa madai
yanayofanana.
Akitolea
mfano wa madai hayo Mkaguzi wa mifumo ya kompyuta kutoka wizra hiyo
alisema yupo mwalimu aliyekuwa akidai Sh. milioni 500, wakati
deni sahihi ni Sh. laki tano.
SERIKALI YASEMA HAKUNA DENI HALALI LA WALIMU AMBALO HALIJALIPWA.
Reviewed by crispaseve
on
12:08
Rating:
Post a Comment