''CHUCK NORRIS'APANDISHWA MAHAKAMANI IRINGA ADAIWA KUHUSIKA KUMJERUHI PAROKO WA RC ISIMANI
Leo polisi walikuwa hana shida na waandishi hata pale ilipoonekana hujawapata vema watuhumiwa walikuwa wakiwaweka sawa ili upate picha nzuri tofauti ya mtuhumiwa wa mauwaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi
Watu saba wakazi wa Isimani wilaya ya Iringa mkoani Iringa wakiongozwa na mtuhumiwa Alex Mgunda maarufu kwa jina la Chuck Norris wamefikishwa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mkoa wa Iringa Juma S.K Hassan na kusomewa makosa 6 likiwemo la kumjeruhi kwa risasi paroko wa Kanisa Katoliki (RC) Isimani wilayani Iringa , Angelo Burgeo (
Watu
saba wakazi wa Isimani wilaya ya Iringa mkoani Iringa wakiongozwa na
mtuhumiwa Alex Mgunda maarufu kwa jina la Chuck Norris leo
wamefikishwa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mkoa wa
Iringa Juma S.K Hassan na kusomewa makosa 6 likiwemo la kumjeruhi kwa
risasi paroko wa Kanisa Katoliki (RC) Isimani wilayani Iringa , Angelo Burgeo ( 60) na msaidizi wake, Herman Myalla (36) kabla ya kumpora fedha kiasi cha Tsh. milioni 2.5 na Euro 1000
Wakili wa Serikali aliwataja watuhumia hao kuwa Joseph Ngwale ( 30 ) ,Alex Mgunda ( 30 ),Joshua Mlagala ( 28 ) wote wakazi wa Isimani, Bruno Mdemu ( 47 ) ambaye ni dereva wa kanisa hilo ,Daud Ngwale ( 24 ),Elasto Ngwale ( 38 ) wakazi wa Isimani na Gaitani Kitwange ( 62 )mkazi wa Mkungugu Iringa
Akiwasomea shitaka la kwanza mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mkoa Juma Hassan, la kula njama ya kutenda kosa , Wakili wa serikali Riziki Matitu alidai kuwa Novemba
15 mwaka huu wote kwa pamoja huko katika kijiji cha Luanja Tarafa ya
Isimani Iringa Vijijini walitenda makosa hayo,ambapo washitakiwa
walikana kosa hilo.
Shitaka la pili lilikuwa la kuvunja nyumba,Wakili Matitu alidai kuwa mnamo Novemba 15 katika kijiji cha Luanja kwenye kanisa la Katoliki la Isimani walivunja na kufanya wizi wa kutumia silaha na kujeruhi.
Wakisomewa
kosa la tatu la unyang’anyi wa kutumia silaha na kuiba sh.milioni 2.8
na Euro 100, Wakili hiyo wa serikali alidai kuwa kabla ya kutenda kosa hilo walimtishia Paroko Angelo Burgeo Kwa silaha na kuchukua fedha hizo,huku kosa la nne na la tano lilikuwa la kujeruhi, ambapo wote k wa pamoja pasipo uhalali walimjeruhi Paroko Angelo Burgeo na Herman Myalla ambaye ni msaidizi wa Paroko huyo .
Aidha
Wakili huyo akisoma shitaka la mwisho ambalo lilikuwa likimkabili
Mshitakiwa wa Kwanza Joseph Ngwale kwa kutuhumiwa kumiliki silaha pasipo
kihalali,Matitu alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alikutwa
nyumani kwake akimiliki silaha bila kibali na hivyo kuchukuliwa hatua za
kisheria.
Kwa upande wake mtuhumiwa namba mbili Mgunda
aliiomba mahakama hiyo kumwondoa katika kesi hiyo kwa madai kuwa yeye
si makazi wa Isimani kama alivyoshtakiwa bali ni mwenyeji wa Isakalilo
mjini Iringa na alikamatwa usiku akiwa nyumbani kwake .
Huku mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo akidai kuwa maelezo aliyotoa alikuwa hajitambui baada ya kupigwa sana na polisi baada ya kukamatwa ,maombi yaliyotupiliwa mbali na mahakama hiyo kwa madai kuwa kukamatwa Isakalilo hakuwezi kukutoa katika kesi ya msingi kwani yawezekana mtuhumiwa akatoka Zanzibar na kuja kuiba Iringa na kukamatiwa huku hivyo kuwataka wasubiri kujitetea kesi hiyo itakapoanzwa kusikilizwa.
Huku mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo akidai kuwa maelezo aliyotoa alikuwa hajitambui baada ya kupigwa sana na polisi baada ya kukamatwa ,maombi yaliyotupiliwa mbali na mahakama hiyo kwa madai kuwa kukamatwa Isakalilo hakuwezi kukutoa katika kesi ya msingi kwani yawezekana mtuhumiwa akatoka Zanzibar na kuja kuiba Iringa na kukamatiwa huku hivyo kuwataka wasubiri kujitetea kesi hiyo itakapoanzwa kusikilizwa.
Kesi
hiyo ambayo ililetwa tena mahakamani hapo Desemba 6 mwaka huu ,na
washitakiwa wamerudi rumande,ambapo katika kesi hiyi kisheria haina
dhamana .
Post a Comment