WAREMBO KUTOKA ULAYA KUSHIRIKI MISS EAST AFRICA 2012
MISS EAST AFRICA BELGIUM- Cynthia Ikwene (24)
Warembo mbalimbali wanaoishi
Ulaya na walioshinda katika mashindano ya Miss East Africa huko Ulaya
pia watashiriki katika mashindano ya Miss East Africa 2012
yatakayofanyika tarehe 07 December katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam warembo hao ni:
1. MISS EAST AFRICA BELGIUM- Cynthia Ikwene (24)
2.MISS EAST AFRICA NETHERLANDS- Mareg Marcos (21)
3.MISS EAST AFRICA FRANCE- Fiona Ruboneka (24)
Fainali za mashindano ya Miss
East Africa 2012 zitashirikisha warembo kutoka Nchi za Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia,
Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu
yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu
Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo
yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja
wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya
Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.
MISS EAST AFRICA FRANCE- Fiona Ruboneka (24)
MISS EAST AFRICA NETHERLANDS- Mareg Marcos (21)
Post a Comment