TAJI LA MISS EAST AFRICA LABAKI TANZANIA HUKU MREMBO JOCELYNE MARO AKINYAKUA TAJI HILO
Mrembo wa
Afrika Mashariki 2012 (Tanzania), Jocelyne Maro (katikati) akiwa na
mshindi wa pili (Uganda),Ayisha Nagudi pamoja na Mshindi wa tatu
(Burundi),Ariella Kwizera mara baada ya kupatikana kwa washindi hao
katika Shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar
es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mshindi
wa taji la Afrika Mashariki Kutoka Tanzania Jocelyne Maro akiwapungia
mkono watazamaji mara baada ya kuvalishwa taji la Afrika Mashariki
usiku wa Kuamkia leo Ndani ya Ukumbi wa Mlimani City
Mrembo wa Afrika Mashariki
2012 (Tanzania), Jocelyne Maro akipongezwa na washiriki wenzie
walioingia kwenye hatua ya tano mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye
Mrembo wa Afrika Mashariki Kwa Mwaka 2012/2013 usiku wa kuamkia leo
Hii ndio tano bora iliyoingia kwenye Kinyang'anyiro Na Hatimaye Kumfanya Mtanzania Kuibuka Mshindi
Warembo wakipita Jukwaa Kwa Mikato Tofauti tofauti
Mshereheshaji Gaetano Kutoka Uganda akiendelea na Majukumu hapo
Eti hawa Wanaitwa Vijana wa Tigo Kisa staili yao ya Kuimba inafanana na tangazo la tigo wabongo bana....The Voice Wonder hao wakifunika mbaya.
Burudani Safi Kutoka Kwa Mad Ice
Bloggers na Waandishi wa habari wakiendelea na kazi ya kurusha matukio live
Hapa mmiliki wa Lukaza Blog (Wa Pili Kushoto) niliponaswa na kamera wakati nikiwajibika Haswa
Wadau mbali mbali walifikika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar kushuhudia Mrembo wa Afrika Mashariki anavyopatikana.
Reviewed by crispaseve
on
10:06
Rating:
Post a Comment