YANGA WAINGIA KAMBINI KATIKATI YA JIJI
VIEWED 367 TIMES
Kikosi cha Young Africans
Baada
ya kuichapa timua ya Azam FC kwa bao 1-0 mwishoni mwa wiki, timu ya
Young Africans Sports Club leo imeingia kambini katika Hoteli ya Tansoma
katikati ya jiji kujiaandaa na mechi inayofuata dhidi ya timu ya Kagera
Sugar, mchezo utakaofanyika siku ya jumatano katika dimba la Uwanja wa
Taifa kuanzia majira ya saa 10 jioni.
Young
Africans ambayo iliwapa furaha washabiki, wapenzi wa soka na wanachama
wake kwa soka safi la ufundi wa hali ya juu, itashuka dimbani kuwakabili
wakata miwa hao ambao katika mchezo wa awal waliibuka na ushindi wa bao
1-0 mchezo uliofanyika katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba.
Young
Africans yenye jumla ya point 39 na mabao 34 ya kufunga na mabao 12 ya
kufungwa itashuka dimba la uwanja wa Taifa kuhakikisha inaibuka na
ushindi katika mchezo huo ili kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya
VPL na hatimaye iweze kutwaa Ubingwa huo.
Mara
baada ya mazoezi ya leo asubuhi, kocha mkuu Brandts amesema anashukuru
vijana wake kwa kufanya kile alichowaagiza, nidhamu ya hali ya juu na
kushika maelekezo yake ndio vitu vilivyopelekea kuendelea kuibuka na
ushindi katika michezo mbali mbali waliyocheza.
Nawapongeza
washabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga waliojitokeza kwa wingi siku
ya jumamosi, kuja kuwashangilia vijana, kikubwa nawaomba waendelee na
moyo huo huou kwani waliwapa nguvu vijana na kuwafanya wacheze kwa
kujiamini mda wote wa mchezo 'alisema Brandts'.
Aidha
Brandts alisema matokeo ya juzi yameendelea kuiweka Yanga katika nafasi
nzuri ya kuelekea kutwaa Ubingwa na atahakikisha wanajitahidi kushinda
kila mchezo ili kujiweka katika mazingia mazuri ya kutwaa Ubingwa wa
Ligi Kuu ya Vodacom.
Kikosi
cha wachezaji 26 na benchi la ufundi wote wameingia kambini katika
Hoteli ya Tansoma mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi na wachezaji wote
ni wazima kiafya na kiakili hivyo hakuna mcheaji hata mmoja ambaye ni
majeruhi.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz
Post a Comment