KENYA YATAMBA KILIMANJARO MARATHON 2013


Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-Moshi
Wanariadha kutoka Nchini Kenya
wameendeleza Umwambawao katika mbio za Nyika za Kilimanjaro ‘Kilimanjaro
Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Wakenya walidhihirisha umwamba
katika Mbio za Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji wao Kipsang Kipkemoi
(pichani) kunyakua nafasi ya kwanza katika mbio hizo za mwaka huu
upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph
aliyebeba Medali ya Dhahabu.
Nafasi ya pili hadi ya tano kwa
wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo Maithiya Loshile
Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice Muchiri, Frida Too, Rosaline
David na Jane Kenyara.
Jumla ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.

Post a Comment