SAFARI LAGER YAFUNGA ZOEZI LA FOMU ZA PROGRAMU YA 'SAFARI LAGER WEZESHWA'
Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa kufunga zoezi la kuchukua na
kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es Salaam
leo mchana.Kulia ni Jaji Mkuu wa Programu hiyo, Joseph Migunda.
***************************
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia bia yake ya Safari Lager leo imefunga rasmi zoezi fomu za ushiriki wa programu ya
wajasiriamali ya “Safari Lager Wezeshwa”
msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alisema kwamba zoezi la fomu za ushiriki wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa msimu
huu tumelifunga rasmi leo. Baada ya hapa fomu hizo zitakusanywa kutoka katika
vituo vyote na kukabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya kuzifanyia kazi.
Bw. Shelukindo aliendelea kufafanua kwamba programu
hii ilipata mafanikio makubwa mwaka jana ambapo iliwawezesha wajasiriamali 54
waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za vitendea
kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili. Alisema, “Upatikanaji
wa fomu hizi ndio mwanzo rasmi wa safari kuelekea uwezeshaji wa wafanyabiashara
wadogo wadogo kwa msimu huu. Safari Lager inatoa fursa kwa mara ya pili, inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya
kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka.
“Safari Lager Wezeshwa”itatoa ruzuku
nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika harakati za
kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaojaza fomu za
ushiriki na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia hasa
ya Safari Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia
mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii.
inayowazunguka”.Alifafanua kwamba
programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio wafanyabiashara
wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu hiini kutoa hamasa kwa
wajasiriamali kote Tanzania ili wajitahidi zaidi katika shughuli wanazofanya na
pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa
msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama fedha taslimu kwa watakaofaulu
vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na
kazi anayofanya.
Naye Bwana Joseph
Migunda, jaji mkuu wa programu ya“Safari
Lager Wezeshwa”kutoka taasisi ya TAPBDS, waratibu wa programu hii alisema
kwamba baada ya fomu kukusanywa zitafikishwa kwao kwaajili ya kuzifanyia kazi
ili kupata wahitaji sahihi kutokana na michanganuo yao jinsi walivyojieleleza
na baada ya hapo watafutwa huko waliko ili kudhibitisha waliyoyaeleza kwenye
fomu zao. Kama ilivyokuwa mwaka jana, washindi msimu huu wa pili watawezeshwa
kwa kupatiwa elimu ya biashara na ruzuku za vitendeakazi mbalimbali kulingana
na biashara zao.
Post a Comment