CRDB BANK YAFANYA HAFLA FUPI UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC NCHINI MAREKANI
Mhe.
Balozi Liberata Mulaula katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa
CRDB Bank Dkt. Charles Kimei wakati wageni wakiingia kwenye hafla fupi
iliyoandaliwa na CRDB kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa
ajili ya kutangaza huduma mpya za kibenki kwa ajili ya Diaspora na
maboresho ya huduma ya Tanzanite.
Waziri
wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiingia kwenye Ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani kulikofanyika hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB
Bank Jumatano Oct 9, 2013 kwa ajili ya kutambulisha huduma mpya za Benki
hiyo kwa ajili ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi.
Mhe.
Balozi Liberata Mulamula akiwatamburisha waheshimiwa wageni kwa baadhi
ya Watanzania walofika kusikiliza huduma mpya za Benki ya CRDB kwa ajili
ya Diaspora na maboresho ya huduma ya Tanzanite na baadae kumkaribisha
mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei kuongea na WanDMV kwa
niaba ya WanaDiaspora.
Mkurugenzi
mkuu wa CRDB Bank, Dkt Charles Kimei akielezea huduma hizo mpya ambazo
ni JIJENGE (Mortgage Finance) na FAHARI HUDUMA (Argent Banking) na pia
alielezea maboresho ya hudma ya Tanzanite ikiwemo mteja anapofkisha
kiasi fulani cha pesa kwenye akaunti yake hakutakuwa na makato ya aina
yeyote yatakayokatwa kila mwezi.
Waziri
wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiongea machache na kuwaambia
wanaDMV wajisikie wapo Tanzania na salama kwani amekuja na ujumbe mzito
unaowakilisha Bara na visiwani na baadae kumshukuru Mhe. Balozi Mulamula
kwa makaribisho mazuri na CRDB Bank kwa kuandaa hafla hiyo fupi
iliyofanyikia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Jumatano Oct 9, 2013
jioni.
Waziri wa Fedha na Uchumi akiongoza ujumbe wake kwenye chakula cha jioni.
Duputy Governor Economic & Financial Policies Dkt. Natu El- maamry Mwamba akijiatia chakula cha jioni.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula nae akijipatia chakula cha jioni.
Kulia
ni Waziri wa Fedha na Uchumi Zanzaibar Mhe. Yussuf Mzee akibadilishana
mawili matatu toka kushoto ni Mariam Mkama, Love Maganga na Tully Esther
Mwambapa ambaye nia Director of Marketing, Reserch and Customer Service
wa CRDB Bank.
Mkurugenzi
mkuu wa TRA Harry Kitilya (kati) akibadilishana mawili matatu na
Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Colonel Adolph
Mutta (kushoto) na Afisa Ubalozi Dkt. Switebert Mkama.( Picha na Vijimambo Blog)
Post a Comment