KUNDI LA BONGO MOVIE LIMEAMUA KUMTENGA WEMA SEPETU KWAKTOKUSHIKI KATIKA MSIBA WA BABA YAKE. SOMA KILICHO SABABISHA
Katika hali isiyotarajiwa katika wasanii wanaounda kundi la Bongo
Movie ambalo linaundwa na baadhi ya wasanii wa filamu Swahiliwood
wamejikuta wakijitenga kushiriki msiba wa baba mzazi wa msanii mwenzao
Wema Isack Sepetu, baada ya kuundwa zengwe na mmoja wa watu wenye
ushawishi katika kundi hilo, Wema akiongea kwa huzuni amesema kuwa hata
wale waliofika jana katika msiba huo hawakufika kwa ajili ya kumfariji
bali walifika kwa ajili ya kumsanifu.
filamucentral.co.tz ilifanya utafiti ili kubaini hilo kwa kuwapigia
simu baadhi ya wasanii wanaotoka katika kundi hilo nao bila kusita kwa
masharti ya kutotajwa majina walitiririka kwa kusema kuwa ni kweli
uongozi wa kundi hilo umetoa agizo watu wasishiriki kutokana na tabia ya
msanii huyo kutoshiriki katika misiba ya wasanii wenzake.
“Ni kweli hilo lipo na lina ukweli kwa njia moja au nyingine Wema
bwana huwa hashiriki katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu
sana na ana sauti katika kundi la Bongo Movie amesema kuwa katika misiba
iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo na Kanumba
kwa sababu alikuwa mtu wake,”anasema kijana huyo.
Hili si jambo la kulifurahia kwa wasanii kwani halijengi bali
linaleta mgawanyiko wa moja kwa moja, msanii mwingine alikiri kuwa Wema
anabagua kushiriki misiba kwani wakati amefariki marehemu John Maganga
alipigiwa simu ili ashiriki katika msiba lakini alisema yupo Location,
hivyo wasanii wenzake wanamtenga ili aone umuhimu wa kushiriki misiba ya
wenzake.
Jana jioni nyumbani hakukuwa na wasanii zaidi ya mtangazaji wa
kipindi cha Take One Zamaradi Mketema akiwa na Rais wa shirikisho la
wasanii Simon Mwakifwamba na waombolezaji wengine, huku baadhi ya
wasanii wakifika pale na kuondoka jambo ambalo Wema alilitafsiri kama
walifika pale kutoa lawama ili asiwaone kama hawajafika lakini hawakuwa
na dhamira ya kweli mioyoni mwao.
KUNDI LA BONGO MOVIE LIMEAMUA KUMTENGA WEMA SEPETU KWAKTOKUSHIKI KATIKA MSIBA WA BABA YAKE. SOMA KILICHO SABABISHA
Reviewed by crispaseve
on
13:31
Rating:
Post a Comment